Tukio hilo ambalo linalenga kuwaleta pamoja wasomaji wa Qur'ani kutoka kote duniani, linawaalika Waislamu wa makundi yote ya rika kushiriki.
Watu wanaopenda kushiriki wanahitajika kuwasilisha klipu ya video ya usomaji wao, usiozidi dakika tatu kwa muda, kwa kamati ya mashindano. Video lazima ianze na mshiriki kutaja jina lake kamili, na inapaswa kuwa bila madoido yoyote ya sauti au taswira, bila kukatizwa au kuhaririwa.
Kwa washiriki walio na umri wa chini ya miaka 16, iwapo watafuzu, wataruhusiwa kuhudhuria mashinano wakiwa wameandamana na mlezi mmoja.
Ili kujiandikisha, washiriki wanaweza kutembelea tovuti rasmi ambayo ni https://alkafeel.net/DeansAward na kufuata hatua zilizoainishwa zikiwemo:
1. Chagua lugha inayofaa.
2. Jaza fomu ya usajili kwa usahihi.
3. Jaza jina kama linavyoonekana kwenye pasipoti.
4. Jaza umri, nchi, na nambari ya mawasiliano ya WhatsApp au Telegram inayotumika.
5. Pakia nyaraka zinazohitajika, ikiwa ni pamoja na video ya qiraa, kopi ya pasipoti, na picha yako iliyo na uwazi.
6. Bonyeza kidude cha usajili na usubiri hadi faili zote zipakiwe kwa ufanisi.
Zaidi ya hayo, washiriki lazima watume video zao za qiraa na taarifa zinazohitajika kwa akaunti ya mashindano katika Telegramu yenye nambari ya +9647760005311. Iwapo kutakuwa na matatizo ya kiufundi na Telegram, wanaweza pia kuwasiliana na nambari hiyo hiyo kupitia WhatsApp.
Majina ya washiriki waliokubaliwa yatatangazwa Januari 15, 2025, na waliofaulu watapatiwa taarifa kwa ajili ya mipango ya kusafiri kwenda Iraq. Kipindi cha kukaribisha washiriki nchini Iraq kimepangwa kati ya Januari 29 na Januari 31, 2025.
Mashindano ya Kwanza ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani ya Al-Ameed, yaliyofanyika hapo awali, yalivutia washiriki kutoka nchi 21.
3491174