IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya Qur'ani ya watoto wa nchi tano za Afrika

15:52 - July 11, 2022
Habari ID: 3475489
TEHRAN (IQNA)- Idara ya Mfawidhi wa Haram ya Hadhrat Abbas AS katika mji wa Karbala, Iraq imeandaa mashindano ya Qur'ani Tukufu ambayo yamewashirkisha watoto na mabarobaro wa nchi tano za Kiafrika.

Kwa mujibu wa tovuti ya Al Kafeel, mashindano hayo ambayo yamefanyika kwa njia ya intaneti yamewaleta pamoja washiriki kutoka Mauritania, Mali, Senegal, Niger na Tanzania.

Mashindano hayo yamesimamiwa na Kituo cha Masomo ya Afrika ambacho kinafungamana na Ofisi ya Masuala ya Kiutamaduni ya Idara ya Mfawidhi wa Haram ya Hadhrat Abbas AS.

Mkuu wa kituo hicho, Sheikh Saad Sattar al Shimri amesema washiriki katika mashindano hayo walikuwa na umri wa miaka 6-15.

Amesema lengo kuu la mashindano hayo ni kuwahimiza watoto na mabarobaro kuhifadhi sura fupi fupi za Qur'ani Tukufu.

Halikadhalika amebaini kuwa, wataalamu wa Qur'ai kutoka Taasisi ya Qur'ani ya Idara ya Mfawidhi wa Haram ya Hadhrat Abbas AS ndio waliokuwa majaji katika mashindano hayo.

Sheikh Saad Sattar al Shimri amesema washindi walitunukiwa zawadi baada ya mashindano na kutokana na mafnaikio makubwa yaliyopatikana kuna mpango wa kuandaa mashindano mengi zaidi katika siku za usoni.

پایان مسابقات قرآنی آستان عباسی با حضور پنج کشور آفریقایی +عکس / اماده

4069923     

captcha