IQNA

Mwezi wa Ramadhani

Vikao 2,500 vya Qur'ani nchini Iran wakati wa Ramadhani

12:01 - March 16, 2023
Habari ID: 3476712
TEHRAN (IQNA) - Jumuiya ya Darul Qur'an al-Karim ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inapanga kufanya duru 2,500 za usomaji wa Qur'ani nchini wakati wa mwezi mtukufu ujao wa Ramadhani.

Hujjatul Islam Ali Taqizadeh, Mkuu wa Jumuiya hiyo aliyasema hayo jana Jumatano katika kikao na waandishi wa habari kilichofanyika hapa mjini Tehran kuhusu programu za Qur'ani zilizopangwa katikak mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Amesema Jumuiya hiyo na vyombo vingine vya Qur'ani Tukufu vinauchukulia Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuwa ndio kilele cha shughuli zao za Qur'ani na kuongeza kuwa, juhudi zitafanywa ili kufanya matukio zaidi ya Qur'ani katika mwezi huu wa Ramadhani hususan katika masuala ya tafsiri ya Qur'ani na kutafakari aya za Kitabu Kitukufu.

Msomi huyo amesema lengo kuu la shughuli za Qur'ani katika Ramadhani ya mwaka huu litakuwa ni Surah Muhammad ya Kitabu kitukufu na kampeni iliyopewa jina la "Muhammad (SAW); Mtume wa Wema".

Hujjatul Islam Taqizadeh ameongeza kuwa Sra hii inaleta matumaini na habari njema ambazo Mwenyezi Mungu anawapa waumini katika sura hii ni miongoni mwa sababu zilizoifanya kuchaguliwa kuwa nguzo ya programu za Qur'ani katika mwezi huu wa Ramadhani.

“Muhammad (SAW); "Nabii wa Wema" itafanyika kwa ushirikiano wa idadi ya mashirika mengine kama Wizara ya Utamaduni na Mwongozo wa Kiislamu, Wizara ya Sayansi, Utafiti na Teknolojia, na Shirika la Wakfu na Masuala ya Hisani, alibainisha.

Kampeni hiyo inajumuisha vipindi vya kufasiri Quran vinavyojumuisha aya za Surah, mashindano ya usomaji wa vitabu, n.k., aliendelea kusema.

Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambao unatazamiwa kuanza Machi 23 mwaka huu ni mwezi wa tisa wa kalenda ya Kiislamu.

Ni kipindi cha sala, saumu, sadaka na uwajibikaji kwa Waislamu duniani kote.

Quran iliteremshwa kwenye moyo wa Mtukufu Mtume (SAW) katika mwezi huu.

Wakati wa Ramadhani, Waislamu hufunga (kujinyima chakula na vinywaji) na kujuzuia na mambo mengine mengi kuanzia macheo hadi machweo.

Pia wanatumia muda mwingi katika mwezi huu kusoma na kutafakari kuhusu aya za Qur'ani Quran.

Nchini Iran, programu mbalimbali za Qur'ani zikiwemo maonyesho, duru za Qur'ani, vikao vya tafsiri ya Qur'ani na mashindano hufanyika kila mwaka katika mwezi mtukufu.

4128305

Habari zinazohusiana
captcha