IQNA

Harakati za Qur'ani

Qari wa Iran anahudhuria Kongamano la Kuhifadhi Qur'ani la Bangladesh

12:27 - December 03, 2024
Habari ID: 3479846
IQNA - Qari mashuhuri wa Iran Hamid Reza Ahmadivafa anashiriki katika kongamano la 23 la kimataifa la Usomaji wa Qur'ani Tukufu nchini Bangladesh.

Kongamano hilo lilizinduliwa wiki hii katika hafla iliyohudhuriwa na maafisa na watu wa Bangladesh pamoja na wawakilishi kutoka balozi za nchi za Kiislamu.

Msikiti wa Kitaifa wa Baitul Mukarram katika mji mkuu Dhaka uliandaa sherehe za ufunguzi.

Katika hotuba yake, Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini Bangladesh Seyed Reza Mirmohammadi alielezea kufanya programu kama hizo kama utangulizi wa kuundwa kwa jamii ya Qur'ani na kuandaa uwanja wa kukuza aya na mafundisho ya Qur'ani.

Vile vile alirejea matukio ya hivi sasa katika ulimwengu wa Kiislamu na akasema Waislamu zaidi kuliko wakati mwingine wowote wanahitaji kufanyia kazi mafundisho ya Qur'an na kuungana kwa mujibu wa amri za Kitabu Kitukufu.

Amelitaja suala la Palestina kuwa ni suala namba moja katika ulimwengu wa Kiislamu na kusema kulitatua na matatizo mengine haiwezekani bila ya kutekeleza maamrisho ya Qur'ani ya kuunda Umma wa Kiislamu ulioungana.

Programu ya kila mwaka ya Qur'ani inaandaliwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani ya Bangladesh, inayojulikana kama 'IQRA'.

Akizungumza katika hafla hiyo, mkuu wa IQRA Sheikh Ahmed bin Yusuf aliwasilisha ripoti kuhusu shughuli na programu tofauti zitakazofanyika wakati wa kongamano hilo.

Kwingineko katika hafla hiyo, Ahmadivafa na  maqari  kutoka Misri, Morocco, Iraq na Pakistan walisoma aya za Quran Tukufu.

Kongamano hilo la wiki mbili litashuhudia vikao vya Qur'ani vinavyofanyika katika miji mikuu ya Bangladesh kama vile Dhaka, Chittagong, Sylhet na Khulna.

3490917

 

captcha