Tangazo hilo limetolewa ikiwa ni katika fremu ya sera za kuanza kuondoa vizuizi ambavyo vilikuwa vimewekwa kuzuia kuenea COVID-19.
Idara ya Miongozo ya Kidini Qatar imetangaza mpango maalumu wa kuanza tena shughuli za vituo hivyo vya kufunza Qur'ani Tukufu ambapo vitarejea kama ilivyokuwa kabla ya janga la COVID-19. Hatahivyo sharti ya kufunguliwa vituo hivyo ni kuzingatia kanunu za kiafya za kuzuia kuenea COVID-19 ikiwa ni pamoja na wanafunzi kutokaribiana darasani, kuvaa barakoa na washiriki wote kupata chanjo kamili ya COVID-19.
Mkuu wa Idara ya Miongozo ya Kidini Qatar Mal-Allah Al Jaber amesema kwa sasa ni vituo 61 tu vya kufunza Qur'ani ndivyo vitakavyofunguliwa na washiriki pia ni wavulana tu. Aidha amewataka washiriki wote wazingatia kanuni na taratjibu zilizowekwa za kuwapokea wanafunzi.