IQNA

Kombe la Dunia Qatar

Neno 'Quran' laongoza katika mitandao ya kijamii + Video

20:28 - November 22, 2022
Habari ID: 3476132
TEHRAN (IQNA)- Hatu ya kusomwa Qur'ani Tukufu katika sherehe za ufunguzi wa Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar uliambatana na sifa nyingi kutoka kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii katika intaneti, kiasi kwamba neno 'Quran' kwa Kiingereza limeongoza kwa siku kadhaa katika maneneo yanayotafutwa katika mitandao ya kijamii hasa Twitter.

Kombe la Dunia la FIFA la 2022 nchini Qatar lilianza Novemba 20 kwa usomaji wa aya ya Qur’ani Tukufu na yamkini hii ni mara ya kwanza katika historia ya kombe hilo.

kilichouteka ulimwengu na kuwavutia watazamaji ni kusomwa aya za Qur'ani Tukufu na msomaji wa Qur'ani mwenye umri wa miaka 20 Ghanim Al Muftah, ambaye pia ni balozi wa FIFA wa Kombe la Dunia.

“Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane.Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi.” inasema sehemu ya aya ya 13 ya Sura al Hujuraat aliyoisoma Ghanim. Inaaminika hii ni mara ya kwanza kwa Kombe la Dunia la FIFA kufunguliwa kwa aya za Qur’ani.

Ghanim kijana mlemavu, aliyezaliwa na hali ya nadra ambayo inadhoofisha ukuaji wa upande wa chini wa mwili, alionekana pamoja na mwigizaji Mmarekani mshindi wa Oscar Morgan Freeman. Muigizaji huyo wa Kimarekani alikaa uwanjani kando ya msomaji Qur’ani (qari) huyo wa Qatari.

Kufuatia utumizi wa aya hiyo ya Qur'ani Tukufu, neno Quran katika Kiingereza liliongoza katika mitandao ya kijamii katika sehemu mbalimbali za dunia.

Watumiaji wa intaneti walisambaza klipi ya usomaji huo wa Qur'ani huku wakionyesha kufurahishwa kwao na hatua hii ya kipekee, ambayo ilionyesha hamu ya Qatar kuakisi dini na utamaduni wake katika Kombe la Dunia.

Watumiaji na wamiliki wa klipu hizi kwenye mitandao ya kijamii walipongeza kuanza kwa hafla ya ufunguzi na programu hii ya Qur'ani ambayo kupitia kwayo waandaaji wa Kombe la Dunia la Qatar 2022 walitaka kuakisi utamaduni na dini ya Uislamu.

Maoni katika mitandao ya kijamii yalionyesha kushangazwa na watazamaji wengi wa hafla ya ufunguzi wa ujumbe wa maelewano, amani na umoja ambao uliwasilishwa kupitia usomaji wa aya za Qur'ani na kijana wa Qatar, na madhumuni yake yalikuwa kukuza utamaduni wa muungano kati ya mataifa, na ushiriki wa mwigizaji wa Mmarekani  mwenye asili ya Afrika katika ufunguzi huo ilikusudiwa kusisitiza suala hili.

Farid Khan, mwandishi wa habari alisema kwenye Twitter: "Sherehe ya ufunguzi wa Kombe la Dunia la Qatar 2022 huko Qatar kwa usomaji wa aya nzuri za Qur'ani Tukufu imejaa ujumbe wa umoja, usawa, maelewano na mshikamano."

Kwa upande wake, mwimbaji Lisa alisema: "Kuishi chini ya hema moja kubwa iitwayo Dunia kwa kuheshimiana na kutohukumu kwa matumaini kwamba tunapata uzuri katika tofauti zetu inaonekana muhimu na ya ndoto wakati huu, umefanya vizuri."

Muthia, mwandishi mwingine wa habari aliandika: "Kufunguliwa kwa Kombe la Dunia la 2022 kwa usomaji wa aya ya Qur'ani ilikuwa ubunifu ambao hakuna mtu angeweza kufikiria mapema. Mabilioni ya watazamaji kutoka kote ulimwenguni walishangazwa na mpango huo wa Qatar, kitu ambacho hakijawahi kutokea katika historia ya miaka 92 ya Kombe la Dunia."

4101449

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha