IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya Qur'ani Qatar yatajumuisha washiriki 1,200 kutoka nchi 67

20:50 - December 21, 2022
Habari ID: 3476283
TEHRAN (IQNA)- Taasisi ya Kijiji cha Utamaduni (Katara) nchini Qatar imetangaza Jumanne kwamba washiriki 1273 watawakilisha nchi 67 za Kiarabu na za kimataifa watashindania toleo la sita la "Tuzo ya Katara ya Kusoma Qur'ani Tukufu".

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kijiji cha Utamaduni (Katara), Khaled bin Ibrahim Al Sulaiti alisema kuwa toleo hili litakalofanyika chini ya kauli mbiu ya “Ipambeni Qur’ani kwa sauti zenu” litashuhudia ushiriki wa washiriki 588 kutoka nchi 19 za Kiarabu na washiriki 685 kutoka nchi 48 zisizo za Kiarabu.

Misri, Sudan na Somalia zinaongoza kwenye orodha ya nchi za Kiarabu zinazoshiriki kwa kuwa na washiriki 280, zikifuatiwa na nchi za Kiarabu za Maghreb zenye 216, eneo la Sham na Iraq zenye washiriki 59 na 33 kutoka mataifa ya eneo  la Ghuba ya Uajemi, aliongeza.

Toleo hili limeshuhudia washindani kutoka nchi zisizo za Kiarabu wakiwazidi wale kutoka nchi za Kiarabu kwa mara ya kwanza katika historia ya tuzo hiyo, pamoja na ongezeko kubwa la idadi ya nchi zisizo za Kiarabu, Al Sulaiti alisema.

Msimamizi mkuu wa tuzo hiyo Khaled Abdul Rahim Al Sayed alisema kuwa washiriki 100 bora wataorodheshwa kwa awamu ijayo huko Doha, huu ukiwa ni mjumuiko wa kwanza baada ya kusimama kwa miaka miwili kutokana na janga la Covid-19.

"Tuzo ya Katara ya Kusoma Qur'ani" inalenga kuhimiza vipaji mashuhuri katika kusoma Qur'ani Tukufu; kugundua, kusaidia na kuwatambulisha watu wenye vipaji duniani; kuheshimu wasomaji mashuhuri na wabunifu wa Qur'ani Tukufu; kuwahamasisha vizazi vijana kushikamana na dini yao, na kutambua wajibu wao kwa imani yao ya Kiislamu.

3481769

captcha