IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Watu zaidi ya 1,300 wajisajili kushiriki Mashindano ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani Qatar

15:57 - January 04, 2024
Habari ID: 3478145
IQNA - Zaidi ya wasomaji au maqari 1,300 wamejiandikisha kushiriki Mashindano ya 7 ya Tuzo ya Kuhifadhi Qur'ani ya Katara

Taasisi ya Cultural Village Foundation, Katara,  ilitangaza kuwa idadi ya washiriki katika mashindano hayo yam waka huu yanayofanyika chini ya kauli mbiu ya “Pambeni Quran kwa sauti zenu,” imefikia 1,315, kutoka nchi 64

Jumla ya waliojisajili kutoka nchi za Kiarabu ni 685, wakiwakilisha nchi 18 za Kiarabu, pamoja na washiriki 630 kutoka nchi 46 zisizo za Kiarabu.

Nchi za eneo la Maghreb, kaskazini mwa Afrika, zinaongoza idadi ya waliojiandikisha ambao ni  307, zikifuatwa na nchi za Misri, Sudan na Somalia ambazo zina waliojisajili 233, kisha zile za Sham na Iraqi zina watu 93 waliojisajili. Wakati idadi ya washiriki kutoka nchi za Ghuba ya Uajemi ilifikia 52.

Kamati ya mchujo itatathmini wote waliojisajili  na hatimaya kuchagua washiriki 100 bora zaidi wa kufuzu kwa hatua ya mchujo, ambayo itafanyika Doha. Washindi 100 watashiriki katika mchujo wa raundi ya saba kupitia vipindi 20 vya televisheni. Katika kila sehemu, washiriki watano wanachuana, na mmoja wao atachaguliwa kuingia katika hatua ya mchujo wa nusu fainali, ambapo washiriki 20 watachuana.

Tuzo ya Katara ya Kusoma Qur'ani inalenga kuhimiza vipaji mashuhuri katika kusoma Qur'ani Tukufu, kuvumbua watu wenye vipaji, kuwaunga mkono na kuwatambulisha kwa ulimwengu, kuwaenzi wasomaji mashuhuri na wabunifu, kuhamasisha vizazi vinavyochipuka kushikamana na dini yao, na kutimiza wajibu wao kuelekea imani yao na ujumbe wa Kiislamu, na inataka kuwahimiza watoto wa Kiislamu kurejea Kitabu cha Mwenyezi Mungu - Mwenyezi - ufahamu, utendaji na kutafakari.

Thamani ya zawadi zilizotengwa kwa ajili ya tuzo ni QR900,000. Mshindi wa kwanza atapata QR500,000, mshindi wa pili, QR300,000, na mshindi wa tatu, QR100,000.

3486677

captcha