IQNA

Qatar kuanzisha vituo zaidi vya Qur'ani vya wanawake

15:25 - March 30, 2021
Habari ID: 3473771
TEHRAN (IQNA) – Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu Qatar imetangaza mpango wa kuanzisha vituo zaidi vya kusomesha wanawake Qur'ani Tukufu nchini humo.

Akizungumza na waandishi habari jumatatu mkuu wa Idara ya Masuala ya Kuhubiri Uislamu na Muongozo katika wizara hiyo Malullah Abdurahma al-Jaber amesema majengo sita yatazinduliwa kwa ajili ya kutoa mafunzo ya  Qur'ani Tukufu kwa wanawake nchini humo.

Ameongeza kuwa kwa ujumla kote Qatar kuna vituo 162 vya serikali vya kutoa mafunzo ya Qur'ani Tukufu kwa wanawake na wanaume. Amesema hivi sasa vituo hivyo vina wanafunzi 22,000.

Ameongeza kuwa idara yake inasimamia vituo hivyo na inahakikisha kuwa kuna waalimu waliohitimu ambao wanatoa mafunzo ya Qur'ani Tukufu.

Naye Muaath Yusuf al Qaasami, mkurugenzi wa kitengo cha Qur'ani na Sayansi za Qur'ani katika idara hiyo ya masuala ya kuhubiri Uislamu na muongozo  amesema kutokana na janga la COVID-19 wanafunzi wengi hawajaweza kujisajili katika masomo. Aidha amesema hivi sasa wako katika mkakati wa kutoa mafunzo kwa maimamu kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

3474325

captcha