Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amemuelezea muuguzi kama malaika wa rehma; na akasema: Katika kipindi cha corona au COVID-19 na katika mazingira magumu mno ya jakamoyo na wasiwasi mkubwa zaidi kuliko ya hali ya kawaida, wauguzi wameweka kumbukumbu ya kazi kubwa na wamejituma na kufanya mambo ambayo kwa kweli ni ya kustaajabisha.
Habari ID: 3473475 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/20