Jinai za Israel dhidi ya Wapalestina Gaza
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametumia ibara ya 99 ya Hati ya Umoja wa Mataifa, ambayo ni nadra sana kutumiwa na Katibu Mkuu wa umoja huo, kulitolea wito mzito Baraza la Usalama wa "kushinikiza kuepusha janga la kibinadamu" katika Ukanda wa Gaza na kuungana katika kutoa wito wa kusitishwa kikamilifu mapigano kati ya utawala wa Kizayuni wa Israel na Harakati ya Mapambano (Muqawama) ya Kiislamu ya Palestina HAMAS.
Habari ID: 3477999 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/07
Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA)- Huku vita vya maangamizi ya kimbari vya utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Gaza vikiendelea, maafisa wa Palestina wanasema ndege za kivita za utawala huo zimelenga maeneo ya karibu na mji wa Khan Yunis kwa kutumia mabomu ya fosforasi ambayo yanakatzwa kwa mujibu wa sheria za kimataifa.
Habari ID: 3477988 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/05
Kadhia ya Palestina
TEHRAN (IQNA)- Hatimaye kumefikiwa makubaliano ya kusitisha vita huko Gaza kwa muda wa siku nne ili kutoa fursa ya kufikishwa misaada ya kibinadamu na pande mbili kubadilishana mateka.
Habari ID: 3477928 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/22
Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA) - Mwanaharakati wa Gaza na mkuu wa shirika la kutoa misaada anasema Wapalestina hawawezi tena kuamini sheria za kimataifa kwani zimeshindwa kuwalinda watoto ambao wanakabiliwa na uvamizi wa kikatili wa Israel.
Habari ID: 3477926 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/21
Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA) – Zaidi ya watoto 5,000 wameuawa katika vita vya mauaji ya kimbari vya utawala katili wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza tangu Oktoba 7. Onyo: Video hii ina matukio ambayo wengine wanaweza kupata ya kuwasumbua.
Habari ID: 3477925 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/21
Watetezi wa Palestina
CANBERRA (IQNA) – Maelfu ya waandamanaji wanaounga mkono Palestina waliandamana kote Australia wikiendi hii, wakitoa wito wa kukomeshwa mara moja kwa mashambulizi ya kinyama ya utawala haramu wa Israel kwenye Ukanda wa Gaza ambayo yameua zaidi ya watu 13,000, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto, tangu Oktoba 7.
Habari ID: 3477918 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/20
Jinai za Israel
RABAT (IQNA) - Shirika la Kiislamu la Elimu, Sayansi, na Utamaduni (ISESCO) limetoa tamko kali siku ya likilaani mashambulizi ya anga ya Israel dhidi ya shule mbili kaskazini mwa Ukanda wa Gaza kuwa ni "fedheha kwa ubinadamu" na "uhalifu wa kutisha".
Habari ID: 3477917 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/20
Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA)- Takriban watu 50 wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa wakati ndege za kivita za utawala wa Israel zilipodondosha mabomu katika msikiti mmoja katika mtaa wa Sabra katikati mwa Ukanda wa Gaza huku utawala huo ukiendeleza mauaji ya halaiki dhidi ya Wapalestina katika eneo hilo.
Habari ID: 3477900 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/16
Jinai za Israel
LONDON (IQNA) - Askofu Mkuu wa Canterbury amesema hakuna msingi wowote wa kimaadili unaoweza kuhalalisha mauaji ya Wapalestina huko Gaza ambayo yanatekelezwa na utawala wa Israel.
Habari ID: 3477889 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/14
Jinai za Israel
AL-QUDS (IQNA) - Mashambulio yasiyokoma ya utawala haramu wa Israel kwenye Ukanda wa Gaza yaliyoanza tarehe 7 Oktoba yamesababisha hospitali 22 na karibu vituo 50 vya afya katika eneo la pwani kuacha kutoa huduma.
Habari ID: 3477885 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/13
Jinai za Israel
GAZA (IQNA)- Kuendelea mashambulizi ya kila upande ya jeshi la Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza na kujiri mapigano makali kati ya vikosi vya muqawama na wavamizi hao karibu na kambi ya al-Shati iliyoko magharibi mwa mji wa Gaza, ni baadhi ya habari za hivi karibuni kutoka Palestina inayokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel.
Habari ID: 3477873 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/10
Jinai za Israel
PRETORIA (IQNA)-Afrika Kusini imeitaka Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) yenye makao yake makuu mjini The Hague (ICC) kuuwajibisha utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na vitendo vyake vya ukiukaji wa sheria za kimataifa wakati utawala huo ukiendelea kufanya jinai dhidi ya binadamu katika Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3477867 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/09
Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA) - Mwandishi mwingine wa habari wa Kipalestina ameuawa katika mashambulizi ya anga ya Israel huko Gaza huku vita vya utawala haramu wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza vikiendelea kwa muda wa zaidi ya mwezi mmoja.
Habari ID: 3477860 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/08
Jinai za Israel
AL-QUDS (IQNA) - Idadi ya misikiti iliyoharibiwa katika mashambulizi ya anga ya utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza inakaribia 50.
Habari ID: 3477815 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/10/30
Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA)- Sambamba na kuanza operesheni ndogo ya nchi kavu ya jeshi katili la utawala haramu Israel kwa lengo la kujipenyeza Ghaza usiku wa kuamkia leo, zaidi ya raia 100 Wapalestina wameuawa shahidi huku utawala huo ukilaaniwa kote duniani kwa kutekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina. Hayo yamejiri huku Umoja wa Mataifa ukitaka vita visitishwe mara moja.
Habari ID: 3477800 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/10/28
Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA)- Ofisi ya Habari ya serikali huko Gaza Palestina imetangaza kuwa, idadi ya Wapalestina waliouawa shahidi tangu utawala haramu wa Israel ulipoanza kufanya mashambulio mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza mnamo Oktoba 7 imepindukia 7000 huku makumi ya maelfu ya wengine wakiwa wamejeruhiwa au kutoweka.
Habari ID: 3477797 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/10/27
Jinai za Israel
AL-QUDS (IQNA) - Vikosi vya Israel vimewabana waumini wa Kiislamu wa Kipalestina katika kitongoji cha Wadi Al-Joz mjini Al Quds (Jerusalem), na kuwazuia kufika Msikiti wa Al-Aqsa kwa ajili ya Sala ya Ijumaa ya kila wiki.
Habari ID: 3477795 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/10/27
GAZA (IQNA) - Idadi ya watu waliouawa katika mashambulizi ya anga ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza imezidi 1,900 huku msafara wa Wapalestina waliokuwa wakielekea kusini mwa Gaza ukilengwa kwa makombora ya Israel.
Habari ID: 3477738 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/10/15
Kadhia ya Palestina
TEHRAN (IQNA)-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema utawala wa Kizayuni wa Israel utachapwa "kibao kikali zaidi" kwa mauaji inayoendelea kufanya dhidi ya wananchi wa Palestina katika Ukanda wa Gaza iliouwekea mzingiro.
Habari ID: 3477707 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/10/10
GAZA (IQNA) - Zaidi ya wakazi 120,000 wa Wapalestina wa Ukanda wa Gaza wameyakimbia makazi yao kutokana na mzozo unaoendelea kati ya vikosi vya upinzani na jeshi la Israel, Umoja wa Mataifa ulisema.
Habari ID: 3477702 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/10/09