IQNA

Jinai za Israel

UN yataka Israel isitishe mapigano mara moja Gaza ili kukomesha mauaji na mateso ya kutisha

18:37 - January 13, 2024
Habari ID: 3478189
IQNA - Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu (OCHR) imesisitiza haja ya kusitishwa mara moja mapigano katika Ukanda wa Gaza ili kumaliza mauaji na mateso ya wananchi wakati vita vya utawala wa Israel dhidi ya eneo hilo vikwa vinakaribia kutimia siku 100.

Kusitishwa kwa mapigano mara moja ni " jambo la dharura zaidi kuliko hapo awali", OHCHR ilisema Ijumaa.

Akizungumza kabla ya vita vya Gaza kutumia siku 100 Jumapili, Msemaji Liz Throssell alisisitiza haja ya wafanyakazi wa OHCHR kufikia maeneo yote ya Eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu kuchunguza ukiukaji wa haki za binadamu.

Wiki 14 zimepita tangu utawala wa Israel uanze kampeni yake ya kikatili ya mauaji na uharibifu katika Ukanda wa Gaza. Zaidi ya Wapalestina ambapo 23,000 wameuawa hadi sasa, wengi wakiwa wanawake na watoto, huku kukiwa na uharibifu mkubwa wa miundombinu ya kiraia ikiwa ni pamoja na nyumba, hospitali, shule,  sehemu za ibada, mifumo ya maji, na vifaa vya Umoja wa Mataifa. Idadi kubwa ya wakazi milioni 2.2 wa Gaza sasa wameyahama makazi yao.

Throssell alikumbusha kwamba Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu Volker Türk amerudia kutoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano "kukomesha mauaji na mateso ya kutisha, na kuruhusu utoaji wa haraka na ufanisi wa misaada ya kibinadamu kwa wakazi wanaokabiliwa na viwango vya kushangaza vya njaa na magonjwa,” na kuongeza kuwa “hili ni jambo la dharura zaidi kuliko wakati mwingine wowote.”

Akizungumzia mwenendo wa uhasama, alisema OHCHR wamesisitiza mara kwa mara namna utawala wa Kizayuni wa Israel unavyokaidi na kupiiza  kanuni za kimsingi za sheria za kimataifa za kibinadamu.

Throssell alilitaka jeshi la utawala wa Israel kuchukua hatua za haraka za kuwalinda raia, kwa kuzingatia sheria za kimataifa.

3486784

Habari zinazohusiana
captcha