IQNA

Jinai ya Israel

Afisa mwandamizi wa Hamas auawa katika hujuma ya kigaidi ya Israel

15:30 - January 03, 2024
Habari ID: 3478137
IQNA-Naibu mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Palestina Hamas ameuawa katika shambulio la kigaidi la ndege isiyo na rubani ya utawala katili wa Israel katika kitongoji cha kusini mwa mji mkuu wa Lebanon wa Beirut.

Siku ya Jumanne kwamba Saleh al-Arouri aliuawa kufuatia mlipuko katika jengo moja katika wilaya ya al-Musharrafieh kusini mwa Beirut.

Arouri aliuawa katika "shambulio la kihaini la Wazayuni," mtandao wa televisheni umesema na kuongeza kuwa mlipuko huo ulitokea baada ya ndege isiyo na rubani ya Israel kulipua jengo hilo kwa makombora matatu na kusababisha vifo vya watu sita.

Hamas ilithibitisha kuuawa shahidi kwa Arouri ambaye alikuwa mkuu wa harakati hiyo ya muqawama  katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na Ukanda wa Gaza uliozingirwa, na kumtaja kuwa "mbunifu" wa Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa.

Hamas iliapa katika taarifa yake kwamba kuuawa shahidi kiongozi huyo "hakutadhoofisha mapambano yanayoendelea" katika Ukanda wa Gaza.

Izzat al-Rishq, mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Hamas, alisema katika taarifa hiyo kwamba, mauaji hayo yanathibitisha kwa mara nyingine kushindwa kabisa kwa adui kufikia malengo yake yote ya kichokozi katika Ukanda wa Gaza."

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya harakati ya Hamas, Ismail Haniyeh amesema utawala haramu wa Israel utawajibika kwa mauaji ya afisa mkuu wa harakati hiyo, Saleh al-Arouri, na ameyataja mauaji hayo kuwa ni "kitendo cha kigaidi na ukiukaji wa mamlaka ya kujitawala ya Lebanon."

Haniyeh aliyasema hayo jana Jumanne, muda mfupi baada ya shambulio la kigaidi la ndege zisizo na rubani za Israel dhidi ya kitongoji cha kusini mwa mji mkuu wa Lebanon, Beirut lililoua shahidi watu sita akiwemo Arouri.
"Tunaomboleza mauaji ya shahidi wa kiongozi wa mapambano na mtu mkubwa wa kitaifa, Sheikh Saleh Al-Arouri, pamoja na makamanda wa Al-Qassam, Samir Fandi na Azzam Al-Aqra' na mashahidi wengine, kufuatia shambulizi la kiuoga la Wazayuni huko Beirut", amesema Haniyeh.

Ameongeza kuwa: "Mauaji ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Al-Arouri na ndugu zake ni kitendo cha kigaidi na ukiukaji wa mamlaka ya kujitawala ya Lebanon, na yanapanua wigo wa uchokozi wake kwa watu wetu na taifa letu."

"Utawala wa Kinazi wa Wazayuni unabeba dhima ya uchokozi huu," aliongeza na kusema: "Damu safi ya Sheikh Saleh al-Arouri na ndugu zake imechanganyika na damu ya makumi ya maelfu ya mashahidi wa Ukanda wa Gaza, Ukingo wa Magharibi, na nje ya nchi."

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas ameendelea kusema kwamba "harakati inayowatoa viongozi na waanzilishi wake kama mashahidi kwa ajili ya hadhi na heshima ya watu na taifa letu haitashindwa kamwe."

Mtandao wa televisheni wa al-Mayadeen nchini Lebanon iliripoti jana Jumanne kwamba Saleh al-Arouri aliuawa kufuatia mlipuko uliotokea katika jengo moja katika wilaya ya al-Musharrafieh kusini mwa Beirut.

Arouri ameuawa katika "shambulio la kihaini la Wazayuni," televisheni hiyo imeripoti na kuongeza kuwa, mlipuko huo ulitokea baada ya ndege isiyo na rubani ya Israel kulipua jengo hilo kwa makombora matatu na umeua watu sita.

3486658

Habari zinazohusiana
captcha