iqna

IQNA

Shambulizi la Israel dhidi ya Bandari ya al Hudaydah
Vikosi vya Jeshi la Yemen vimeapa kuendeleza operesheni zinazoiunga mkono Palestina baada ya utawala haramu wa Israel kushambulia maeneo ya raia katika nchi hiyo ya Kiarabu.
Habari ID: 3479160    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/07/21

Kadhia ya Palestina
Makundi ya kisiasa na kijamii ya Palestina yamepongeza uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) wa kutazama ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu na Israel la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kuwa haramu na kinyume cha sheria.
Habari ID: 3479153    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/07/20

Jinai za Israel
IQNA-Idara ya Habari ya Serikali ya Palestina katika Ukanda wa Ghaza imesema, askari wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel wamefanya "shambulio la kikatili ambalo halijawahi kushuhudiwa kwenye kambi ya wakimbizi ya Nuseirat" na kuua kwa umati Wapalestina 210 hadi hivi sasa na makumi ya watu kujeruhiwa mitaani.
Habari ID: 3478951    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/06/09

Jinai za Israel
IQNA - Maafisa wa Palestina na makundi ya muqawama wamekaribisha uamuzi wa Umoja wa Mataifa wa kuuongeza utawala wa Israel kwenye 'Orodha ya Aibu' kwa kuua watoto katika vita vya Gaza.
Habari ID: 3478950    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/06/08

IQNA - Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imetoa onyo kali kwamba misaada ya kutosha ya kibinadamu haiwafikii Wapalestina huko Gaza, na kusababisha visa vikali vya njaa miongoni mwa watoto.
Habari ID: 3478924    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/06/04

Jinai za Israel
IQNA-Rais wa Venezuela amezilaani Marekani na Umoja wa Ulaya kwa kutofanya lolote kukomesha mauaji "ya kutisha" na ya Kinazi ya Israel dhidi ya Wapalestina.
Habari ID: 3478899    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/05/29

Muqawama
IQNA-Abu Obeida, Msemaji wa Brigedi za Izz ad-Din al-Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS ametangaza kuwa, wapiganaji wa brigedi hizo wamekinasa kwa kukiwekea chambo chini ya handaki kikosi cha jeshi la Kizayuni na kufanikiwa kuwaangamiza, kuwajeruhi na kuwakamata mateka askari kadhaa wa jeshi hilo katika eneo la kambi ya Jabalia kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3478891    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/05/27

Jinai za Israel
IQNA-Jeshi katili la utawala wa Kizayuni wa Israel limeshambulia kwa makombora kambi ya watu waliolazimika kuhama makazi yao na kuhamia eneo lililotengwa kuwa na usalama huko Rafah, na kuwaua shahidi Wapalestina wasiopungua 40, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto.
Habari ID: 3478890    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/05/27

Jinai za Israel
IQNA-Zaidi ya watoto 15,000 wanaripotiwa kuuawa shahidi na jeshi la utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza huko Palestina.
Habari ID: 3478832    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/05/16

Jinai za Isarel
Mkuu wa timu ya Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) ametahadharisha kuwa mazingira ya kuidhaminia Gaza maji safi, chakula na dawa za matibabu yamefika marhala hatari na kwamba hatua ya kukifunga kivuko cha Rafah kunaifanya hali ya wakazi wa ukanda huo kuwa mbaya zaidi.
Habari ID: 3478796    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/05/09

Jinai za Israel
IQNA-Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imeitaka jamii ya kimataifa ichukue hatua na kuubebesha dhima utawala wa Kizayuni wa Israel, kutokana na jinai na mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala huo haramu dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3478780    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/05/06

Jinai za Israel
IQNA-Afisa wa Umoja wa Mataifa anasema uharibifu uliosababishwa na vita vya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza haujawahi kuonekana tangu Vita vya Pili vya Dunia, huku akikadiria kuwa ujenzi mpya wa eneo hilo la Palestina unaweza kuchukua miaka 80 na kugharimu hadi dola bilioni 40.
Habari ID: 3478771    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/05/04

Jinai za Israel
IQNA: Wakati kukiwa na ongezeko la wito wa kimataifa kwa Israel kujizuia na mashambulizi zaidi Gaza na ripoti za Mei Mosi za mashambulizi mengine mabaya, wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wamesisitiza kuhusu athari mbaya zinazoendelea za vita hiyo na haja ya kuhakikisha njia za kuaminika za usambazaji wa misaada kwa watu wanaohitaji kwa udi na uvumba zinapatikana.
Habari ID: 3478756    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/05/02

Jinai za Israel
IQNA-Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Afrika Kusini imetoa mwito wa kufanyika uchunguzi wa haraka na wa kina kuhusu makaburi ya umati yaliyogunduliwa katika Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3478737    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/26

Jina za Israel
IQNA - Msemaji wa Umoja wa Mataifa ameitaja ripoti kuhusu kugunduliwa kwa makaburi ya halaiki huko Gaza kuwa ni ya kushtusha, huku ushahidi wa awali ukionyesha utawala haramu wa Israel umehusika katika jinai hiyo.
Habari ID: 3478724    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/23

Jinai za Israel
IQNA - Takriban miili 190 imetolewa kwenye kaburi la umati katika Hospitali ya Nasser katika mji wa Khan Younis kusini mwa Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3478717    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/22

Jinai za Israel
IQNA - Umoja wa Mataifa umeonya kuhusu hali mbaya katika Ukanda wa Gaza ambapo watu wanahangaika maisha kila siku, ukitangaza kuwa utazindua ombi la kimataifa la dola bilioni 2.8 kwa Gaza na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.
Habari ID: 3478694    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/17

Jinai za Israel
IQNA-Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Palestina, idadi ya mashahidi wa mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza imefikia 33,545 huku utawala huo katili ukiendeleza vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya eneo hilo lililozingirwa.
Habari ID: 3478672    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/12

Jinai za Israel
IQNA-Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina, Hamas, amethibitisha habari ya kuuawa shahidi watoto na wajukuu zake katika shambulio la kinyama la utawala wa Kizayuni na akasema: "kwa machungu haya na kwa damu hii tunajenga matumaini, mustakbali na uhuru wa watu wetu, piganio letu na taifa letu".
Habari ID: 3478669    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/11

Jinai za Israel
IQNA-Viongozi wa dunia wameendelea kulaani kitendo cha wanajeshi wa Israel kuwaua Wapalestina 116 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 760 waliokuwa wakisubiri msaada wa chakula katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa siku ya Alhamisi.
Habari ID: 3478438    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/02