IQNA

Jinai za Israel

Utawala wa Israel umeshambulia Gaza kwa tani 65,000 za vilipuzi ndani ya siku 89

21:16 - January 05, 2024
Habari ID: 3478150
IQNA – Utawala katili wa Israel umefyatua zaidi ya tani 65,000 za makombora na mabomu kwenye Ukanda wa Gaza tangu Oktoba 7, 2023, na kuua takriban watu 22,438, wengi wao wakiwa wanawake na watoto.

Hayo ni  kulingana na ripoti ya Ofisi ya Habari ya Serikali ya Gaza (GMO) ambayo imesema kuwa ndege za kivita za Israel zilidondosha zaidi ya makombora 45,000 na mabomu makubwa, mengine yakiwa na uzito wa hadi pauni 2,000, kwenye eneo ndogo la pwani lenye watu wengi, zikilenga kwa makusudi maeneo yote ya makazi.

Ripoti hiyo iliongeza kiasi cha vilipuzi vilivyodondoshwa na jeshi la Israel kwenye Ukanda wa Gaza kilipita tani 65,000, ambayo ni zaidi ya uzito na nguvu ya mabomu matatu ya atomiki kama yale yaliyorushwa na Marekani kwenye mji wa Hiroshima Japan mwaka 1945."

Ofisi ya Habari ya Serikali ya Gaza pia ilisema kwamba "theluthi mbili ya mabomu na makombora ni yale yasiyoerevu ambayo yanayojulikana kama mabomu bubu." Ilisema kwamba matumizi ya mabomu hayo yalionyesha mashambulizi ya kiholela na kukusudia kuharibu maeneo ya raia.

Ripoti hiyo imebaini kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel umetumia takriban aina tisa za makombora ambayo yamepigwa marufuku kimataifa dhidi ya raia.

Utawala ghasibu wa Israel ulianzisha vita dhidi ya Gaza ili kukabiliana na operesheni ya Okotoba 7  ya harakati zake za wapigania ukombozi wa Palestina au wanamuqawama ambao walikuwa wakilipiza kisasi jinai za zaidi ya miaka 75 za utawala huo katili.

Hata hivyo, licha ya kushambulia Gaza kwa kiasi kikubwa cha mabomu, Israel imeshindwa kufikia malengo yake yoyote iliyotangazwa, kama vile kuwalazimisha watu kukimbilia nchi jirani au kuangamiza kundi la upinzani la Hamas ambalo limechaguliwa na Wapalestina kuongoza Gaza.

3486686

Habari zinazohusiana
captcha