Msikiti wa Jamia wa Moscow umetambuliwa kama msikiti mkubwa zaidi barani Ulaya. Ujenzi wa msikiti huo, ambao umefanyika kwenye eneo ulipokuwepo msikiti mdogo wa kale wa zaidi ya miaka 100, umechukua muda wa miaka 10 hadi kukamilika. Msikiti huo uliogharimu dola milioni 180 kujengwa una ghorofa sita na utakuwa na uwezo wa kuchukua waumini elfu kumi.
Habari ID: 3383099 Tarehe ya kuchapishwa : 2015/10/08