Ayatullah Muhammad Ali Movahhedi Kermani ameongeza kuwa, timu ya mazungumzo ya nyuklia ya Iran inapasa kulipatia kipaumbele suala la kulindwa thamani za mapinduzi, izza na utukufu wa Kiislamu. Akieleza kwamba wananchi wa Iran wanataka mazungumzo yafanyike kwa uwazi kabisa, Ayatullah Kermani amesisitiza kuwa, timu ya mazungumzo ya Iran haipasi kulipatia kundi la 5+1 mwanya wa kuamua walitakalo. Ayatullah Kermani ameshangazwa na msimamo wa kiadui wa Marekani wa kuizuia Jamhuri ya Kiislamu ya Iran isishiriki kwenye mazungumzo ya Geneva 2 yanayojadili mgogoro wa Syria na kuongeza kuwa, siyo shani kabisa kwa nchi kubwa na yenye ushawishi kama vile Iran isishiriki kwenye mazungumzo hayo. Akizungumzia harakati zinazodi kuongezeka za makundi ya kigaidi na yale yanayowakufurisha Waislamu wengine katika nchi za Kiislamu kama vile Iraq na Syria, Khatibu wa sala ya Ijumaa ya mjini Tehran amesisitiza kuwa wanachuoni na maulamaa wa ulimwengu wa Kiislamu na wapenda haki kote ulimwenguni wana jukumu la kuzifichua njama za watenda jinai. Ayatullah Kermani amelaani mauaji wanayofanyiwa Waislamu wa Madhehebu ya Shia katika baadhi ya nchi za Kiarabu kunatokana na propaganda chafu za watawala wa nchi hizo waliokuwa na chuki dhidi ya Mashia, na kuongeza kuwa jinai hizo zinaonyesha wazi undumakuwili wa baadhi ya viongozi wa nchi za Kiarabu.
1352882