IQNA

Zarif: Vikwazo havibadilishi sera za Iran

9:13 - January 14, 2014
Habari ID: 1358688
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema vikwazo havijaweza kibadilisha sera za Jamhuri ya Kiislamu. Amongeza kuwa ni kosa kudhani kuwa Iran imeamua kubadilisha sera zake kutokana vikwazo ilivyowekewa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran aliyasema hayo Jumamosi tarehe 11 Januari  mjini Tehran wakati alipokutana  na Pat Breen, Mwenyekiti wa Kamati ya Sera za Kigeni na Biashara katika Bunge la Kitaifa la Ireland (Oireachtas). Zarif aliongeza kuwa  uhusiano wa Iran na Ireland unaweza kuimarishwa hasa katika nyanja ya biashara. Zarif alisema safari za wabunge wa nchi za Ulaya Tehran ni ishara ya kuwa Magharibi inataka kuimarisha uhusiano na Jamhuri ya Kiislamu. Aliendelea kusema kuwa kuwa safari hizo zinaashiria irada ya pande zote mbili kuimarisha uhusiano.

Breen kwa upande wake amesema Ireland ina azma ya kuimarisha uhusiano wa kisiasa na kibiashara na Iran.

1357691

captcha