Hayo yamesemwa na Sheikh Nabil Qauq, Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Utendaji la Harakati ya Hizbullah nchini Lebanon wakati akizungumza Jumatatu usiku katika khitma ya siku ya saba ya kuuawa shahidi Yusuf Hassan Hafidh, mjini Beirut.
Akiashiria makundi ya kigaidi kama vile al Qaeda amesema kuwa: "Watu wale wale ambao wanatenda vitendo vya kigaidi kwa jina la al Qaeda huko Iraq, Syria, Yemen, Misri, Somalia, Afghanistan na Pakistan sasa wameingia Lebanon."
Kiongozi huyo mwandamizi wa Hizbullah ameonya kuhusu njama za kuibadilisha Lebanon kuwa makao ya magaidi wa Kiwahabi na kusema: "Ugaidi wa kitakfiri hauna dini na wala si dhehebu bali ni shari kamili na ni shari mutlaki na ni tisho kwa watu wote."
1370299