IQNA

Wanajeshi wa Kizayuni wavamia Msikiti wa Al Aqswa

11:33 - February 08, 2014
Habari ID: 1372231
Askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameendeleza unyama wao,

, baada ya kuwashambulia kwa maguruneti, mabomu ya kutoa machozi na risasi za plastiki waumini wa dini ya Kiislamu waliokuwa wakitekeleza ibada ya Sala ya Ijumaa hapo jana ndani ya Masjidul Aqswa huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Taarifa zinasema kuwa, kwa akali watu 20 walijeruhiwa kwenye tukio hilo wakiwemo watoto na wanawake kadhaa. Taarifa zinasema kuwa, askari wa Kizayuni licha ya kuwatia mbaroni vijana kadhaa, waliwakamata na kuwapiga wanawake wasiokuwa na hatia yoyote ile. Shambulio hilo linajiri ikiwa umepita karibu mwezi mmoja, tokea Uri Ariel Waziri wa Ujenzi na Makazi wa Israel alipotangaza mipango mipya ya kuiyahudisha Quds Tukufu kwa kujenga hekalu badala ya Masjidul Aqswa, Kibla cha kwanza cha Waislamu. Matamshi ya waziri huyo wa Israel yamekabiliwa na radiamali kali kutoka kwa wananchi wa Palestina na mataifa mengine ya Kiislamu.
1372016

captcha