Ayatullah Muhammad-Ali Muvahidi Kermani amesema kuwa, kila umma wa Wairani unapojitokeza kwa wingi katika maandamano ya terehe 22 Bahman (11 Februari) ya kuadhimisha sherehe za ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ndivyo maadui wa Jamhuri ya Kiislamu wanavyokosa matumaini na kusononeka. Aidha ameashiria jinai za Marekani dhidi ya wananchi wa Iran baada ya Mapinduzi ya Kiislamu na kusema kwamba, Wamarekani bado hawajaacha kuiwekea Iran mashinikizo ya kiuchumi na kisiasa na wanaendelea kuzusha madai yasiyo na msingi na ya uongo ili wazuie maendeleo ya taifa hili.
Ayatullah Muhammad-Ali Muvahidi Kermani sambamba na kutoa mkono wa pongezi kwa mnasaba wa maadhimisho ya Alfajiri Kumi za ushindi wa Mapinduzi na kumbukumbu ya kumuenzi Imam Khomeini (M.A), amesema maandamano ya Bahman 22 kila yanapokuwa makubwa, huwafanya maadui wazidi kukosa matumaini.
Katika upande mwingine Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran ameashiria uungaji mkono wa Marekani kwa jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina na kusema kwamba, uungaji mkono wa nchi za kibeberu kwa Israel hautofanikiwa kuvunja irada ya harakati ya mapambano ya wananchi wa Palestina.
1371874