Rouhani ameyasema hayo Jumamosi mjini Tehran wakati alipokutana na balozi mpya wa Qatar Tehran Ali bin Hamad al-Sulaiti. Rais wa Iran amesisitiza kuhusu umuhimu wa uhusiano mzuri baina ya nchi jirani kwa ajili ya mustakabali mwema. Amesema Iran iko tayari kuimarisha uhusiano na Qatar katika sekta za uchumi, utamaduni, biashara na fedha. Naye balozi al-Sulaiti amemkabidhi rais Rouhani salamu za kiongozi wa Qatar, Amir Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani na kusema Doha inataka kuboresha uhusiano na Tehran. Rais Rouhani pia amekutana na balozi mpya wa Oman nchini Iran Saud bin Ahmed bin Khalid Al Barwani. Katika mkutano huo, rais wa Iran amepongeza uhusiano mzuri wa Tehran na Muscat hasa katika sekta ya uchumi. Rouhani amesema ushirikiano mzuri wa Iran na Oman ni kwa maslahi ya uthabiti wa eneo. Balozi Al Barwani amempa rais wa Iran salamu za kiongozi wa Oman Sultan Qaboos bin Said Al Said na kusema nchi yake inakaribisha suala la kuimarisha uhusiano na Iran.
1372418