Akitoa hotuba za sala iajUmaa katika mji mkuu wa Bahrain, Manama, Sheikh Qasim amekosoa vikali baadhi ya nchi za Kiarabu ambazo zimebakia kimya mbele ya jinai za Israel huko Ghaza kutokana na kuwa zinataka kuhifadhi nafasi yao mbele ya maadui wa umma na Uislamu.
Akiashiria Siku ya Kimataifa ya Quds, Sheikh Qassim amesema hii ni siku ya Palestina ambayeo imesahauliwa katika aghalabu ya nchi za Kiarabu ambazo zimejidhalilisha mbele ya maadui. Ameongeza kuwa kuhuisha Siku ya Kimataifa ya Quds kunamaanisha kuhuisha kadhia ya Palestina na kuinua hadhi ya Quds na Msikiti wa Al Aqsa katika fikra za umma wa Kiislamu. Amesema kwa kuzingatia kuwa utawala haramu wa Israel unatekeleza jinai ya kuwaua kwa umati watoto, wanawake na watu wasio na hatia huko Ghaza, mwaka huu siku ya Quds ilikuwa na maana maalumu.
Sheikh Qassim pia ameashiria jinai za utawala wa Aal Khalifa nchini Bahrain na kuongeza kuwa utawala huo unabomoa misikiti, unazuia harakati a kidini na kuwazuia watu kuswali katika misikiti kadhaa. Aidha amesema utawala dhalimu wa Aal Khalifa umewafunga gerezani na kuwabaidisha wanazuoni kadhaa wa Kiislamu.