IQNA

Marekani, mshirika mkuu wa jinai za Wazayuni dhidi ya Wapalestina

19:48 - August 02, 2014
Habari ID: 1435160
Huku utawala wa Kizayuni wa Israel ukiendeleza jinai za kivita na mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wasio na ulinzi wala hatia huko katika Ukanda wa Ghaza, Marekani imejitokeza wazi kuunga mkono kwa hali na mali jinai za utawala huo bandia.

Baada ya kupita siku 26 za hujuma ya kinyama ya Israel huko Ghaza, bado hakuna muelekeo wowote wa kuashiria kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel utafungamana na mapatnao ya usitishwaji vita. Punde baada ya kufikiwa mapatano ya usitishwaji vita kwa masaa 72 siku ya Ijumaa, utawala wa Kizayuni ulivunja mapatano hayo ambapo hadi sasa idadi ya waliouawa shahidi na kujeruhiwa Ghaza ni zaidi ya elfu 10.

Mara hii hakuna shaka kuwa Marekani haifichi tena uungaji mkono wake wa kisiasa na hata kijeshi kwa  vita vya kinyama vya Israel dhidi ya Ghaza.  Kwa muda wa wiki nne sasa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa halijachukua hatua yoyo ya maana dhidi ya jinai za kivita za Israel na badala yake limekuwa likitii matakwa ya Marekani. Hii ni pamoja na kuwepo ushahidi wa wazi na ripoti za taasisi za kimataifa kuhusu jinai za kivita za Israel dhidi ya watu wasio na ulinzi Ghaza.  Utawala wa Kizayuni wa Israel umekuwa uakitumia vifaru, makombora na ndege za kivita za Marekani aina ya F16 na F22 kuwashambulia watu wa Palestina. Baadhi ya mashirika ya haki za binaadamu yameshindwa kuendelea kunyamaza kimya kwa kuhofia kupoteza itibari yao. Kwa mfano Shirika la kutetea haki za bainaadamu la Amnesty International limelaani jinai za utawala wa Kizayuni huko Ghaza na kuitaka serikali ya Mareknai ichukue hatua za haraka za kuishinikiza Israel isitishe jinai zake dhidi ya Wapalesitna. Pamoja na hayo wizara ya ulinzi ya Marekani Pentagon imetangaza wazi kuwa itaendelea kuupatia kila aina ya silaha utawala wa Kizayuni wa Israel. Mbali na kutoa msaada huo wa silaha za maangamizi ya umati kwa Israel, Marekani pia imesema itaupatia utawala huo dhalimu msaada wa dola milioni 62. Brian Wood anayhusika na masuala ya udhibti wa silaha katika Amnesty International amesema Marekani inakiuka sheria za kimataifa kwa kuendelea kuipa Israel silaha kwani inaisaidia katika jinai zake huko Ghaza. Marekani ni  nchi inayopeleka idadi kubwa zaidi ya silaha Israel. Takwimu zinaonyesha kuwa tokea mwezi Januri hadi Mei mwaka huu, Marekani imeipatia Israel msaada wa dola milioni 27 kujenga vituo maalumu vya kurushia makombora, dola milioni 9.3 kwa ajili ya kunuanua makombora ya kisasa yanayoongozwa kwa mbali na karibu dola milioni moja kwa ajili ya kununua maroketi, risasi, gurunedi na silaha nyingine ndogo ndogo. Amnesty International inasema tokea Israel ianzishe hujuma yake ya kinyama dhidi ya Ghaza, hadi sasa Wapalestina wasiopungua 1,700 wameuawa shahidi ambapo aghalabu yao ni raia wasio na ulinzi wakiwemo watoto wachanga, wanawake na wakongwe. Utawala huo wa Kizayuni pia umebomoa mahospitali, shule, misikiti, makanisha, vituo vya umeme, mabomba ya maji, mabarabara na kuharibu mashamba katika hujuma yake ya kinyama dhidi ya Ghaza. Jinai hizo zote zimefanyika kwa uungaji mkono wa hali na mali wa Marekani. Kumetolewa miito ya kufikishwa watawala katili wa Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC lakini kutokana na ushawishi mkubwa wa Marekani katika mahakama hiyo na taasisi zingine za kisheria kimataifa, hakuna matumaini ya watenda jinai Wazayuni kufikishwa kizimbani. Ni miaka 66 sasa tokea utawala bandia wa Israel uundwe kwa kukaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina. Katika kipindi hicho chote Marekani imekuwa ndio muungaji mkono mkuu wa utawala haramu wa Israel na imekuwa mshirika nambari moja katika jinai na mauaji ya kimbari ambayo yamekuwa yakitekeleza na Wazayuni dhidi ya watu wa Palestina.

1435009

captcha