Baraza hilo limetaja kitendo cha Daesh cha kumuua kwa kukata kichwa mwanahabari Mmarekani eti kwa jina la Uislamu kuwa ni unyama na ukatili usiokubalika katika Uislamu wala dini yoyote ile ya mbinguni. Baraza Kuu la Waislamu nchini Uingereza aidha limesema limeshangazwa kusikia mwanachama wa Daesh aliyetekeleza mauaji hayo dhidi ya James Foley ni raia wa Uingereza na kutoa wito kwa yeyote anayemfahamu katili huyo kutoa taarifa kwa polisi. Foley ameuawa baada ya Marekani kushindwa kulipa kikomboleo cha mamilioni ya dola kwa magaidi hao.
Baadhi ya wachambuzi wanasema ingawa kuuawa Foley ni tukio la kusikitisha, lakini hayo ni matunda inayovuna Washington kutokana na nafasi yake ya kuanzisha na kufadhili kundi hilo la kitakfiri miaka kadha iliyopita huko nchini Syria.