Baraza hilo lilitoa fatwa rasmi siku ya Ijumaa kufuatia matukio mabaya na ya umwagaji damu yaliyotokea hivi karibuni katika mkoa wa Sweida. Fatwa hiyo ilitoa hukumu za kidini zinazosisitiza utakatifu wa damu, mshikamano wa kijamii, kuepuka fitina, na marufuku ya kutafuta hifadhi kwa adui.
Ilisema mojawapo ya kanuni zisizopingika za Uislamu ni marufuku ya usaliti na kushirikiana na adui Mzayuni ambaye ni mwovu, na marufuku hii ni kali zaidi katika miezi mitakatifu.Ikitaja Aya ya 190 ya Surah Al-Baqarah, “Na piganeni katika njia ya Mwenyezi Mungu dhidi ya wale wanaowapigana nanyi, lakini msizidi kiasi, maana Mwenyezi Mungu hawapendi wale wanaozidi,” ilisema uadui wa utawala wa Israeli ni jambo thabiti na halisi.Baraza hilo pia limesisitiza kuwa kuwauwa watoto na wanawake, kushambulia raia wasio na hatia na wanyonge, na kuwahama makazi yao ni marufuku, bila kujali dini au kabila lao.Baraza la Fatwa la Syria liliendelea kusema kuwa serikali ina wajibu wa kulinda raia wote bila ubaguzi, kuanzisha usalama, kuzuia fitina, na kusaidia majeruhi.Baraza pia liliwahadharisha watu juu ya hatari kubwa ya hotuba za kikabila na za kuchochea na kuwaomba watu kuthibitisha ukweli wa habari kabla ya kuamini au kuichapisha na kuepuka chochote kinachosababisha mgawanyiko na chochezi.Taasisi ya dini ya Syria ilimalizia kwa kuitaka amani, kuokoa damu, na kuepuka fitina, na kuweka jukumu la kudumisha umoja wa kitaifa na utulivu kwa makundi yote ya watu wa Syria.
Hayo yanajiri wakati ambao,
Rais wa mpito wa Syria na waziri mkuu wa Israel wamekubaliana kusitisha mapigano kufuatia makabiliano ya umwagaji damu ya siku kadhaa katika Jimbo la Suweida, lililoko kusini mwa Syria.
Mjumbe Maalumu wa Marekani nchini Syria na balozi wake nchini Uturuki Tom Barrack ametangaza kuwa, Rais wa mpito wa Syria, Ahmed al-Sharaa na Waziri Mkuu wa utawala wa Israel Benjamin Netanyahu wamekubaliana kusitisha vita kufuatia mapigano katika Jimbo la Suweida, kusini mwa Syria,
Jimbo hilo limeripotiwa kuungwa mkono na Uturuki, Jordan, na mataifa mengine jirani, kwa mujibu wa mtandao wa telisheni ya wa Al-Mayadeen.
Barrack amehimiza makundi yote ya kidini na kikabila, ikiwa ni pamoja na Druze, Mabedui, na Sunni, kuweka chini silaha zao na kushirikiana kwa ajili ya kuunda Syria moja iliyoungana.
Shirika linalojiita Syrian Observatory for Human Rights limeripoti kwamba, idadi ya vifo huko Suweida kabla ya kusitishwa mapigano hayo ilikuwa imeongezeka hadi watu 718.
Hata hivyo, Wizara ya Afya ya Syria imetangaza kuwa, watu 260 wamepoteza maisha huku 1,698 wakijeruhiwa katika mapigano hayo ya hivi karibuni.
3493896