IQNA

Maulamaa wa Ulimwengu wa Kiislamu wamtembelea Kiongozi hospitalini

21:38 - September 10, 2014
Habari ID: 1448995
Maulamaa na wanazuoni wanaoshiriki katika Kongamano la Kimataifa la 'Maulamaa wa Kiislamu Wanaounga Mkono Harakati ya Muqawama ya Wapalestina leo wamekwenda hospitalini hapa Tehran kumjulia hali Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Kati ya wanazuni hao alikuwemo Sheikh Naeem Qassim Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon ambaye pia amewasilisha kwa Kiongozi Muadhamu salamu za kumuombea dua na kumtakia afya na umri mrefu kutoka kwa Sayyid Hassan Nasrallah, ambaye ni katibu Mkuu wa harakati hiyo. Wengine waliofika hapo hispitalini ni Ayatullah Asef Mohseni kutoka Afghanistan, Sheikh Sadruddin Qabanchi Imamu wa Sala ya Ijumaa  mjini Najaf al Ashraf nchini Iraq,  Sayyid Ali Fadhlullah kutoka Lebanon, Sheikh Ahmad Sambi rais wa zamani wa Visiwa vya Komoro, Sheikh Ahmad Az Zain Mkuu wa Jumuiya ya Maulamaa Waislamu wa Lebanon na Sheikh Alaadin Zaatry Naibu Mufti wa Syria.

Viongozi na maafisa wa Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu pia wanaendelea kumtembelea Kiongozi Muadhamu Hospitalini. Ikumbukwe kuwa Jumatatu asubuhi Kiongozi Muadhamu alifanyiwa upasuaji wa tezi kibofu (prostate) katika hospitali moja ya umma mjini Tehran na operesheni hiyo ilifanyika kwa mafanikio makubwa. Daktari Marandi, mkuu wa timu ya madaktari wa Kiongozi Muadhamu amesema mara nyingi wagonjwa wote wanaofanyiwa upasuaji wa aina hiyo hubakishwa hospitalini kwa muda wa siku tatu hadi tano ili kuangaliwa hali zao na jambo hilo

1448822

captcha