IQNA

Kiongozi Muadhamu amteua Sarafraz kuwa mkuu mpya wa IRIB

20:59 - November 08, 2014
Habari ID: 1471116
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amemteua Dakta Muhammad Sarafraz kuwa Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) kwa kipindi cha miaka mitano.

Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei leo amemteua Muhammad Sarafraz, aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha matangazo ya ng’ambo ya IRIB kuwa Mkuu wa Shirika hilo akichukua nafasi ya Mhandisi Ezzatollah Zarghami aliyemaliza muda wake. Katika uteuzi wake huo, Kiongozi Muadhamu ameashiria majukumu ya kihistoria ya Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kuhifadhi na kuinua mamlaka ya kiutamaduni na utambulisho wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na kusisitiza kuwa, Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu lina jukumu muhimu sana la kuongoza na kusimamia Utamaduni na Fikra za Jamii na hivyo taasisi hiyo ni sawa na Chuo Kikuu cha Umma chenye jukumu la kueneza kwa wananchi dini, matumaini, ufahamu na mtindo wa maisha ya Kiislamu na Kiirani. Ayatullah Khamenei amesema kuwa, Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran likiwa kama injini yenye harakati na inayoshajiisha maendeleo ya nchi, lina jukumu la kutoa msukumo wa kihabari wa pande zote na linabeba katika mabega yake jukumu la kufanya ubunifu na vile vile kuhamasisha umma na kusaidia viongozi wa utendaji katika kudhamini malengo pamoja na kutekeleza siasa kuu za Mfumo na kufanikisha hati ya malengo ya muda mrefu ya Iran.../mh

1470961

captcha