Kwa mujibu wa gazeti la Uholanzi la De Telegraaf likimnukulu afisa wa usalama wa Ulaya ambaye hakutaka jina lake litajwe na ambaye anafanya kazi katika mojawapo wa balozi za Ulaya mjini Tel Aviv, Israel ilipanga kutumia kombora la kisasa lenye uwezo wa kulenga shabaha kwa ustadi mkubwa likiongozwa kutoka mbali kwa kutumia ndege isiyo na robani. Taarifa zinasema Israel ilikuwa imepanga kutumia kombora ambalo pia lina uwezo mdogo wa uharibifu ili ionekana kana kwamba hujuma hiyo imetekelezwa na mlipuaji wa kujitolea muhanga mwenye mshipi wa bomu.
Imedokezwa kuwa utawala wa Kizayuni ulipanga kutekelelza hujuma hiyo katika Siku ya Ashura, tarehe 10 ya Muharram mwaka huu wa1436 Hijria. Katika siku hiyo Waislamu hukumbuka kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume Muhammad SAW, Imam Hussein AS na wafuasi wake 72 katika mapambano ya Karbala.
Afisa huyo wa usalama kutoka Ulaya amedokeza kuwa Israel ilishindwa kutekeleza hujuma hiyo kwa sababu ya matatizo ya kilojistiki na pia kutokana na teknolojia ya kisasa kabisa inayotumiwa na kikosi maalumu cha walinzi wa Sayyid Nasrallah.
Gazeti hilo la Uholanzi limedokeza kuwa makomandoo Hizbullah wana kofia maalumu ambazo zimeuganishwa kieletroniki na raada maalumu zilizo katika eneo la Jabal Sheikh ambazo hutuma habari za haraka pale ndege yoyote inapoingia Lebanon.Gazeti hilo limedai kuwa Russia imeikabidhi Hizbullah teknolojia hiyo ya kisasa ya kujihami.../mh