IQNA

Mumbai kuwa mwenyeji wa makongamano matatu ya Kiislamu

13:47 - November 02, 2008
Habari ID: 1703263
Mji wa Mumbai huko India utakuwa mwenyeji wa makongamano matatu ya Kiislamu katika mwezi huu wa Novemba.
Gazeti la Times of India limeandika kuwa kongamano la kwanza la kimataifa ambalo litakua na anuani ya "Wanawake wa Kiislamu" litafanyika tarehe 7 Novemba likisimamiwa na taasisi ya Iqra sambamba na kuanza kwa ijtimai ya siku tatu wa Waislamu wa madhehebu ya Suni wa India. Kongamano la tatu la Kiislamu katika mwezi huu wa Novemba ni lile lililoanza tarehe 14 Novemba mjini Mumbai na litaendelea na shughuli zake kwa kipindi cha siku kumi. Kongamano hilo linajadili masuala ya kielimu na Kiislamu.
Lengo la makongamano yote matatu limetajwa kuwa ni kueneza moyo wa maelewano na amani na kuzia kuenea kwa fikra za kufurutu mipaka.
Mumbai ni makao makuu ya jimbo la Maharashtra na ndiyo mji wenye jamii kubwa zaidi ya watu nchini India. 313787
captcha