IQNA

Sherehe za uzawa wa Imam Redha (AS) zafanyika Saudi Arabia

16:09 - November 10, 2008
Habari ID: 1706762
Sherehe za kumbukumbu siku ya kuzaliwa Imam Ridha (AS) zimefanyika Jumatatu katika ukumbi wa kidini (Husseiniya) wa al-Abbasiya katika mji wa Hufuf nchini Saudi Arabia.
Kwa mujibu wa mtandao wa habari wa Rasd , hafla hiyo iliandaliwa na kamati ya Al Auhadiya ya mji wa Hufuf katika mkoa wa Al Ahsa’a na kuhuduriwa na Mashia pamoja na wapenzi wa Imam huyo mjukuu wa Mtume SAW.
Kamati ya Al Auhadiya ya Hufuf imesema katika ujumbe uliotolewa kwa munasaba wa kumbukumbu ya kuzaliwa Imam wa nane kati ya Maimamu 12 ambao ni nuru ya Wilaya kuwa, hafla hii ilianza saa moja jioni kwa saa za Saudi Arabia.
Katika hafla hiyo, mashairi ya kuwasifu Ahlul Bayt (AS) yamesomwa na Mostafa Al Hassan, Abdullah Khamis, na Jawad al Mazidi. 317620
captcha