Kwa mujibu wa gazeti la Star, kikao hicho kimefanyika kwa ushirikiano wa Baraza la Waislamu wa Malaysia na mashirika yasiyo ya kiserikali nchini humo. Sheikh Nur Qadut Mfuti wa jimbo la Juhur amehutubia mkutano huo na kusema kuwa, hii leo vijana Waislamu wanakabiliwa na matatizo mengi ya kijamii na kuna haja ya kutumia mafunzo ya Kiislamu kukabiliana na matatizo hayo.
Mwanchuoni huyo ameashiria zama zilizopita ambapo Uislamu ulinawiri na kusema, baadhi ya Waislamu na hasa vijana wamesahau misingi yao ya kiutamaduni, kielimu na kisayansi na wanaiga utamaduni wa Kimagharibi, suala ambalo litawaathiri vibaya'.
Mufti Nur Qadut amewaambia vijana Waislamu wa Malaysia ambao wanasoma katika nchi za Magharibi kuwa, 'nyinyi mnapaswa kujifunza teknolojia na sayansi walionayo Wamagaribi na wala si nukta potofu za utamaduni wao'.
Akimaliza hotuba yake, ameelezea matumaini kuwa mashirika yasiyo ya kiserikali ya Kiislamu yatawasaidia vijana badala ya kuwakosoa tu. 318263