IQNA

Kikao cha Waislamu na Wakristo huko Wales, Cardiff

10:46 - November 12, 2008
Habari ID: 1707383
Waislamu na Wakristo wa Wales huko UK wanakutana wiki hii kwa lengo la kujadili masuala ya ulimwengu wa sasa na jamii ya nchi hiyo.
Mwandishi wa IQNA ameripoti kuwa, mkutano huo ambao unafanyika chini ya anwani ya "Changamoto za Mustakbali na Jinsi ya Kufikia Mtazamo wa Pamoja", unaanza leo katika mji mkuu wa Weles, Cardiff.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kiislamu ya Wales Salim Kadawi amesema, kuwa na mtazamo wa pamoja ambako ni katika juhudi za kufikia umoja wa kidini, ni zoezi bora la kivitendo la kutekeleza mafunzo ya dini yetu.
Mkutano huo umeandaliwa na Kanisa la Wales, Baraza la Waislamu na Kituo cha Masuala ya Kimataifa cha nchi hiyo.
Wales ni nchi ndogo iliyoko kusini magharibi mwa kisiwa cha Britain ambacho pamoja na Uingereza, Scotland na Ireland ya Kaskazini zinaunda nchi kubwa ya Ufalme wa Muungano wa Britania na Eire ya Kaskazini. Wales ina jamii ya watu karibu milioni tatu na wakazi wake wanazungumza Kiingereza na Kiwales. 318796
captcha