IQNA

Maonyesho ya sita ya nguo za Kiislamu Malaysia

10:33 - November 18, 2008
Habari ID: 1709490
Maonyesho ya Sita ya nguo za Kiislamu nchini Malaysia yatafanyika kuanzia tarehe 24 hadi 27 Novemba katika mji wa Kuala Lumpur.
Kwa mujibu wa gazeti la NSB, kutakuwa na wanamitindo 44 wa nguo za Kiislamu kutoka Indonesia, India, Iran, Dubai Singapore Bangladesh, Pakistan na Ufilipino.
Kupitia maonyesho hayo, Malaysia inatarajia kutagazwa kama mji mkuu wa mitindo ya nguo na mavazi ya Kiislamu duniani. Aidha kuna mpango wa kutoa zawadi kwa lengo la kuhimiza ubunifu mpya wa mavazi ya Kiislamu.
Shah Rezza mmoja wa waandalizi wa maonyesho hayo amesema kuwa: "Tunataka kuonyesha utamaduni wa Kiislamu kwa miundo mbali mbali. Kuwa Muislamu hakumaanishi usivae mavazi mazuri".
Vile vile pembizoni mwa maonyesho hayo kutakuwa na warsha wa kutoa mfunzo kuhusu miundo na ushonaji nguo za Kiislamu. Aidha washiriki watajadili njia za kuanzisha masoko ya nguzo za Kiislamu.
Malaysia ni nchi ya Kiislamu ambayo imepiga hatua kubwa kimaendeleo katika nyanja mbali mbali hasa za teknolojia. 321765
captcha