IQNA

Kuanza mipango ya Wiki ya Muamko wa Kiislamu mjini London

10:14 - November 19, 2008
Habari ID: 1710064
Mipango ya Wiki ya Muamko wa Kiislamu imenza kutekelezwa mjini London ambapo wanafikra na viongozi wa kidini wanahudhuria.
Shughuli za wiki hii zimeanza Jumatatu iliyopita kwa nara ya 'kuenziwa thamani za pamoja za Uingereza' ambapo tovuti maalumu ya upashaji habari za wikii hii imezinduliwa kwa ajili ya kutumiwa na wanafunzi. Shahid Malik, Waziri wa Sheria wa Uingereza amesema katika sherehe za ufunguzi wa shughuli hizo kwamba, kuna habari nyingi potofu zinazoenezwa na vyombo vya habari vya nchi za Magharibi kuhusiana na mafundisho ya Kiislamu, na kwamba kwa kurejea katika tovuti hiyo ambayo imeanzishwa kwa mnasaba wa wiki hii ya muamko wa Kiislamu, vijana wanaweza kupata habari sahihi kuhusiana na mafundisho halisi ya Kiislamu. Amesema kuwa huenda si rahisi kupata habari hizo kwingineko na kuelezea matumaini yake kwamba habari zinazopatikana katika tovuti hiyo zitasaidia sana katika kunyanyua kiwango cha ufahamu wa jamii za Magharibi kuhusiana na Uislamu. Vilevile Dhahur Qureishi, mkuu wa jamii ya Waislamu wa Uingereza amesema katika sherereza za ufunguzi wa wiki hii kwamba, kuna umuhimu mkubwa wa kuarifishwa na kubainishwa kwa mafundisho halisi ya Uislamu ulimwenguni na hasa kufuatia matukio ya Septemba 11 nchini Marekani na yale ya mjini London. Amesema, umuhimu huo unatokana na ukweli kwamba, kuna habari nyingi potofu ambazo zimeenezwa ulimwenguni kuhusiana na Uislamu na Waislamu na hivyo kutoa picha mbaya na isiyofaa dhidi ya ulimwengu wa Kiislamu. Ameongeza kwamba, kuna udharura wa kufanyika mazungumzo kati ya dini mbalimbali kuhusiana na thamani za pamoja za kidini ili kutoa sura halisi ya Uislamu ambao unahubiri amani, upendo, usamehevu na ushirikiano na wafuasi wa dini nyinginezo. 322197
captcha