IQNA

Pazia la al Kaaba kubadilishwa siku ya Arafa

10:58 - November 23, 2008
Habari ID: 1711423
Mkuu wa masuala ya msikiti mtukufu wa Makka na msikiti wa Mtume huko Madina mesema kuwa pazia la nyumba na al Kaaba litabadilishwa siku ya Arafa ambayo itasadifiana na tarehe 18 Mfunguo tatu Dhilhija.
Gazeti la Arab News limeandika kuwa Mkuu wa Masuala ya Msikiti Mtukufu wa Makka (Masjidul Haram) na Msikiti wa Madina (Masjidunnabi) Saleh bin Abdurahman al Hasiin atakabidhiwa pazia jipya la al Kaaba kutoka kwa mtunza pazia la nyumba hiyo ya Mwenyezi Mungu tarehe 29 Novemba.
Pazia jipya la al Kaaba litawekwa kwenye nyumba hiyo kongwe ya Mwenyezi Mungu siku ya Arafa baada ya al Kaaba kuoshwa kwa marashi halisi kutoka Kashani, Iran.
Pazia jipya la al Kaaba lililogharimu Riyali milioni 20 za Saudi Arabia limetayarishwa na kushonwa kwa kutumia kilogramu 670 za hariri halisi na kilogramu 150 za dhahabu na fedha. Pazia hilo pia limenakshiwa kwa aya za Qur’ani na wasanii waliotumia nyuzi za dhahabu na fedha kutimiza kazi hiyo.
Pazia hilo linaundwa na sehemu tatu ambazo ni pazia la mlango wa al Kaaba, kitambaa cha chini ya pazia na pazia asili la nyumba hiyo ya Mwenyezi Mungu.
Vipande 47 vya vitambaa ambavyo kila kimoja kina urefu wa mita 14 na upana wa semtimita 101 vumetumika kutayarisha pazia hilo. 323897
captcha