IQNA

Maonyesho ya “Vyombo vya Habari na Mazungumzo Baina ya Dini” Beirut

11:09 - November 27, 2008
Habari ID: 1713188
Maonyesho ya saba ya vyombo vya habari vya Kikristo chini ya anuani ya: “Vyombo vya Habari na Mazungmzo Baina ya Dini” yanafanyika huko Beirut Lebanon.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA nchini Lebanon, gazeti la Al Mustaqbal la nchi hiyo limetaja sababu ya kufanyika maonyesho hayo, ambayo yameandaliwa kwa hisani ya Kadinali Nasrallah Peter Sfeir Askofu wa Wakristo Wamaronite kwa ushirikiano na Jumuiya ya Kimataifa ya Wakatoliki ya vyombo vya habari, kuwa ni kuimarisha ushirikiano wa vyombo vya habari vya Wakristo. Aidha maonyesho hayo yanalenga kuunga mkono vyombo vya habari vya Kikristo nchini humo na kuhuisha turathi za Lebanon na Mashariki na kuziarifisha kama sehemu ya utamaduni wa maelewano na uhuru.
Kundi la Kiislamu la Leqaa Online linashiriki katika maonyesho hayo ambayo pia yatamuenzi Sheikh Muhammad an-Naqri kutoka Darul Fatwa tawi la Chuo Kikuu cha Al Azhar nchini Lebanon.
Mwakilishi wa Liqaa Online , Kasrwan Abdullah amesema lengo la kushiriki katika maonyesho hayo ni kukuza utamaduni wa mazungumzo na kuwakubali wengine. Amesema mazungumzo baina ya dini nchini Lebanon na kuyatekeleza katika jamii ni jambo linalowezekana. Ameongeza kuwa nchini Lebanon mabawa mawili ya Uislamu na Ukristo yanaweza kujenga nchi huru na kutuma risala hiyo katika jamii nyinginezo.
326214

captcha