Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, msemaji wa Jumuiya ya Utamaduni ya Kiislamu ya Wales Kusini, Latif Khan amesema kuwa ujenzi wa kituo hicho cha Kiislamu umekuwa ni jambo la dharura kutokana na idadi kubwa ya Waislamu mjini humo.
Ameendelea kusema kuwa: ‘Tunahitajia kituo cha Kiislamu kwa ajili ya harakati za Kiislamu na Qur'ani, kuandaa karamu za kidini na kuandaa programu maalumu kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramahani’.
Latif Khan amesema, hazina ya ujenzi wa kituo hicho ilikuwa ni Paundi laki moja na eflu 10 na kwamba Paundi 60 elfu zimepatikana kutoka misaada ya Waislamu watenda kheri. 326349