Hayo yamesemwa na Barakat, muhadhiri wa masuala ya falsafa ya Kiislamu katika chuo kikuu cha Damascus nchini Syria. Ameyasema hayo katika siku ya pili ya kikao cha ‘fikra ya pamoja ya wanachuo wa Ulimwengu wa Kiislamu’ mjini Tehran. Huku akisisitiza kwamba umoja na mshikamano wa Waislamu utapelekea kufichuliwa na kushindwa kwa njama za Marekani dhidi ya Waislamu, Ustadh Barakat amesema kuwa, Waislamu wana wasiwasi mkubwa kuhusiana na kuenea satuwa na ushawishi wa Marekani katika nchi za Kiislamu kwa sababu jambo hilo bila shaka litagonganisha na kuwagawa Waislamu katika makundi tofauti hasimu. Ameashiria umuhimu wa kuwepo muamko wa Waislamu katika kukabiliana na njama za nchi za Magharibi dhidi ya Waislamu na kuongeza kuwa, umoja na mshikamano unapaswa kuimarishwa miongoni mwa Waislamu kupitia mazungumzo. Amesema, nchi za Ulaya zinaungana kwa ajili ya kulinda maslahi yao na kwamba, nchi za Kiislamu ambazo wananchi wao wana itikadi na imani inayofanana, zinapasa kuwa mstari wa mbele katika kuimarisha umoja miongoni mwa Waislamu na hatimaye kuungana. 326959