IQNA

Disemba 8 ni Idul Adh'ha Kyrgyzstan

9:43 - December 07, 2008
Habari ID: 1716548
Jumuiya ya Maulama Waislamu nchini Kyrgyzstan imetangaza Jumatatu tarehe 8 Disemba kuwa sikukuu ya Idul Adh'ha nchini humo. Kwa mujibu wa ripota wa IQNA katika mji mkuu wa Kyrgyzstan, Bishkek, Idara ya Jumuiya ya Maulamaa nchini humo imetangaza pia siku hiyo itakuwa siku ya mapumziko.
Itakumbukwa kuwa Uislamu uliingia Kyrgyzstan kati ya karne 9-12 Miladia. Lakini hadi karne ya 17 Uislamu ulikuwa hauna nafasi muhimu sana katika jamii. Katika karne hiyo Uislamu ulichukua nafasi kubwa zaidi katika maisha ya kila siku ya Wakyrgyzstan.
Wakaazi walio wengi wa Kyrgyzstan ni Waislamu wa madhehebu ya Sunni na kama walivyo Waislamu wengine nchini humo, husherehekea Idi za Kiislamu kwa shamrashamra na katika sikukuu ya Idul Adha huchinja na kufanya ziara katika kaburi la Nabi Suleiman AS.
Kyrgyzstan ni Jamhuri ya zamani ya Shirikisho la Sovieti na iko katika Asia ya Kati. Nchi hiyo ambayo haipakani na bahari, imejaa milima na inapakana na Kazakhstan upande wa kaskazini, Uzbekistan upande wa magharibi, Tajikistan upande wa kusini magharibi na China upande wa mashariki.
Kyrgyzstan ilijinyakulia uhuru wake kutoka Shirikisho la Sovieti Agosti 31 mwaka 1991 na baada ya hapo kulishuhudiwa mwamko mkubwa wa Kiislamu hasa miongoni mwa vijana wa nchi hiyo. 330135

captcha