Bismillahir Rahmanir Rahim
Kama ilivyo kwa kila mwaka, hivi sasa pia ardhi ya wahyi imekuwa mwenyeji wa kundi kubwa la waumini. Nyoyo zenye shauku kutoka kila kona ya dunia, hivi sasa ziko katika ardhi ambayo ni kitovu cha Uislamu na Qur’an, wameshughulika kutekeleza ibada tukufu ya Hijja ambapo kama mtu atazingatia basi atashuhudia ndani yake somo la kubakia milele la Uislamu na Qur’ani kwa ajili ya mwanaadamu na kumfanya apige hatua kubwa za maana za kutekeleza somo na mafundisho yaliyomo ndani yake.
Lengo la somo hilo kubwa ni kutenda mema na kupata heshima mwanaadamu na njia yake ni ya malezi ya watu wema na kujenga jamii salama kwa ajili ya mwanaadamu ambaye anamwabudu Mungu Mmoja ndani ya moyo na roho yake na ambaye anajitakasa na shirki na uchafu wa kimaadili na upotofu na kujenga jamii ambayo muundo wake ni wa uadilifu, uhuru, imani, uchangamfu na dalili zote nyingine za uhai na maendeleo.
Kipengee muhimu katika amali ya Hijja kimefungamana na malezi hayo ya mtu binafsi na jamii kwa ujumla. Tangu wakati wa kuvaa vazi la Ihram na kujitoa mtu katika zile sifa maalumu za mtu binafsi na kuacha matamanio yake mengi na vivutio vyake vya kinafsi hadi kufikia katika Tawaf nembo ya tauhidi na sala katika Maqamu ya Ibrahim mvunja sanamu na mwenye kujitolea mhanga na kumaliza amali ya mwendo wa kukimbia baina ya milima miwili hadi kutulia katika uwanja wa Arafa katikati ya kundi kubwa la wenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu wa kila rangi na kizazi hadi kupitisha usiku wa kumtaja na kuomba dua katika Mash’arul Haram na mfungamano wa kipekee wa kila moyo na Muumba wake sambamba na kuwepo katikati ya mjumuiko huo mkubwa ulioshikamana na baadaye kwenda katika Mina na kumpiga mawe shetani, na kisha amali iliyojaa maana ya kuchinja na kutoa kafara, kuwalisha maskini na wasafiri walioishiwa na mafunzo mengine mengi ndani yake.
Katika mjumuiko wa mambo hayo ndani yake mumekusanyika kwa upande mmoja ikhlasi na unyofu na kuuweka mbali moyo na starehe za kimaada, na kwa upande mwingine juhudi na bidii za kudumu na vile vile mfungamano na kuweko faragha na Allah na aidha mshikamano na uano na maumbile, na pia kuulea na kuujenga moyo na kwa upande mwingine kupigania umoja na mshikamano ndani ya umma adhimu wa Kiislamu na kwa vile vile unyenyekevu mbele ya Allah, na kwa upande mwingine umadhubuti na uimara katika kupambana na batili na vile vile kuujaza moyo mapenzi ya akhera na wakati huo huo kuweka azma thabiti ya kuipamba dunia. Yote hayo yana mafunzo makubwa yanayopaswa kutekelezwa kivitendo.
رَبَّنَا آتِنَا فِی الدُّنْیَا حَسَنَةً وَفِی الآخِرَةِ حَسَنَةً وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ
Mola wetu Mlezi, tupe duniani mema, na Akhera mema, na utulinde na adhabu ya Moto! (al Baqarah 2:201).
Ni kwa sababu hiyo ndio maana al Kaaba Tukufu na ibada ya Hijja kiujumla ikawa chemchemu ya nguvu na uwezo wa jamii chemchemu ambayo imejaa faida na matumizi bora kwa wanaadamu:
جَعَلَ اللَّهُ الْكَعْبَةَ الْبَیْتَ الْحَرَامَ قِیَامًا لِّلنَّاسِ
Mwenyezi Mungu ameifanya Al Kaaba, hii Nyumba Tukufu, ni simamio la watu... (al Maida 5:97).
لِیَشْهَدُوا مَنَافِعَ لَهُمْ وَیَذْكُرُوا اسْمَ اللَّهِ فِی أَیَّامٍ مَّعْلُومَاتٍ
Ili washuhudie manufaa yao na walitaje jina la Mwenyezi Mungu katika siku maalumu… (al Hajj 22:28).
Waislamu kutoka kila nchi, taifa na kizazi hivi sasa wanapaswa kudiriki, kutumia na kuthamini zaidi faida na umuhimu wa faradhi ya Hijja kuliko wakati mwingine wowote kwani mustakbali ulio mbele ya umma wa Kiislamu leo hii uko wazi zaidi kuliko wakati mwingine wowote na matumaini ya kuweza kufikia malengo yaliyowekwa na Uislamu kwa ajili ya mtu binafsi na jamii ya Kiislamu kiujumla yameongezeka zaidi hivi sasa kuliko huko nyuma. Kama katika karne mbili zilizopita umma wa Kiislamu uliporomoka na kushindwa na utamaduni wa kimaada wa Magharibi na aidiolojia za kukana uwepo wa Mwenyezi Mungu kwa pande zake zote mbili za kushoto na kulia, hivi sasa na katika karne hii ya 15 ya mwaka wa Hijria, ni adiliolojia za kisiasa na kiuchumi za Magharibi ndizo zilizokumbwa kwenye tope na zimedhoofika na zinaporomoka na kushindwa, huku Uislamu kutokana na istikama ya Waislamu ukiwa unarejesha utambulisho wake ambapo kufuatia kudhihiri fikra ya tauhidi na mantiki ya uadilifu na umaanawi, Uislamu umeanza kipindi kipya cha ustawi, kuchanua na heshima yake.
Wale watu ambao huko nyuma, na wala si nyuma sana, walikuwa wakiimba wimbo wa kuvunjika moyo ambao si kwa Uislamu na Waislamu pekee bali walikuwa wakidhani msingi mzima wa umaanawi na kupenda dini umeangamizwa na hujuma na mashambulizi ya ustaarabu wa Magharibi, leo hii wanashuhudia kunawiri Uislamu na kupata uhai mpya Qur'ani na Uislamu na wakati huo huo maadui wakizidi kudhoofika na kutoweka pole pole. Watu waliokuwa na mtazamo hasi hivi sasa wanaliukubali uhakika huo kwa moyo na ndimi zao.
Ninasema nikiwa na matumaini kamili kwamba huu ni mwanzo tu, na ahadi kamili ya Mwenyezi Mungu yaani ushindi wa haki dhidi ya batili, ukarabati wa umma wa Qur’ani na ustaarabu mpya wa Kiislamu, iko njiani.
وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَیَسْتَخْلِفَنَّهُم فِی الأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَیُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِی ارْتَضَى لَهُمْ وَلَیُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا یَعْبُدُونَنِی لا یُشْرِكُونَ بِی شَیْئًا وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَلِكَ فَأُولَئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ
“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walioamini miongoni mwenu na wakatenda mema ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyowafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia dini yao aliyowapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watakaokufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu. (an Nur-55)
Ishara za ahadi hiyo iliyotimia katika awamu zake za awali ni ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran na kuasisiwa mfumo wa Kiislamu ambao umeifanya Iran kuwa kituo imara cha fikra, utawala na ustaarabu wa Kiislamu. Tukio hilo la kimuujiza lilitukia wakati fikra za kimaada na za kupiga vita Uislamu za mirengo ya kulia na kushoto ya kifikra na kisiasa ilipokuwa kileleni. Wakati huo mapambano na kusimama kidete Mapinduzi ya Kiislamu mbele ya mapigo ya kisiasa, kijeshi kiuchumi na kiproganda kutoka pande zote kulihuisha matumaini katika dunia ya Kiislamu na kuleta ari na vuguvugu katika nyoyo. Kadiri wakati unavyopita ndivyo umadhubuti na ukakamavu huo unavyozidi na kuimarisha matumaini zaidi kwa nguvu na uwezo wake Mola.
Katika kipindi chote cha miongo mitatu ya baada ya tukio hilo, eneo la Mashariki ya Kati, na nchi za Waislamu za Asia na Afrika zimekuwa uwanja wa mpambano huo wa ushindi. Palestina na Intifadha ya Kiislamu na kusimama kwa dola la Kipalestina na la Kiislamu, ushindi wa kihistoria wa harakti ya Hizbullah na mapambano ya Kiislamu dhidi ya utawala wa kidhalimu, katili na Kizayuni, Iraq na kuasisiwa serikali ya Kiislamu na ya wananchi juu ya maghofu ya utawala wa kikafiri na kidikteita wa Saddam, Afghanistan na kushindwa kwa fedheha wavamizi wa Kikomunisti na utawala kibaraka wao, kushindwa na kufeli kwa mipango yote ya kibeberu ya Marekani ya kutaka kudhibiti Mashariki ya Kati, matatizo na migogoro isiyokuwa na tiba ya ndani ya utawala ghasibu wa Kizayuni, kupanuka kwa wimbi la Uislamu katika nchi nyingi au zote za eneo hili hususan kati ya vijana na wasomi, maendeleo ya kustaajabisha ya kisayansi na kiteknolojia katika Iran ya Kiislamu licha ya vikwazo na mzingiro wa kiuchumi, kushindwa wapenda vita wa Marekani katika medani za kisiasa na kiuchumi, hisia za kupata utambulisho za Waislamu waliowachache katika nyingi ya nchi za Magharibi, yote hayo ni dalili za wazi za ushindi na ustawi wa Uislamu katika mapambano dhidi ya maadui katika karne hii yaani karne ya 15 Hijria.
Ndugu zangu wapenzi! Ushindi huo ni matokeo ya jihadi na ikhlasi. Kwani pindi sauti ya Mwenyezi Mungu iliposikika kutoka katika koo za waja wake, na wakati hima na nguvu za wapiganaji jihadi katika njia ya haki zilipoingia katika medani, na pindi Waislamu walipotekeleza ahadi zao kwa Mwenyezi Mungu, wakati huo Mwenyezi Aliyetukuka na Muweza pia alitimiza ahadi yake na mwenendo wa historia ulibadilika:
وَأَوْفُواْ بِعَهْدِی أُوفِ بِعَهْدِكُمْ
“Na tekelezeni ahadi zangu nitatekeleza ahadi zenu”. (Baqara 40)
یَا أَیُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَنصُرُوا اللَّهَ یَنصُرْكُمْ وَیُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ
Enyi Mlioamini! Mkiinusuru dini ya Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithubutisha miguu yenu”. (Muhammad-7)
وَلَیَنصُرَنَّ اللَّهُ مَن یَنصُرُهُ إِنَّ اللَّهَ لَقَوِیٌّ عَزِيزٌ
Na bila shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anayesaidia dini yake, hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye kushinda. (Al haj-40)
إِنَّا لَنَنصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِی الْحَیَاةِ الدُّنْیَا وَیَوْمَ یَقُومُ الأَشْهَادُ
“Na bila shaka Sisi tutawanusuru Mitume wetu na wale walioamini katika maisha ya dunia na siku watakaposimama mashahidi (Ghafir-51)
Lakini huu bado ni mwanzo tu. Mataifa ya Waislamu yana kazi pevu mbele yao. Kupita katika njia hizo ngumu hakuwezekani ila kwa imani, ikhlasi, matumaini, Jihad, busuri na subira. Njia hii haiwezi kuchukuliwa kwa kupoteza matumaini, kuwa na mitazamo hasi, kutojadli, kutokuwa na hima, kukosa subira, na kuwa na haraka na kupoteza imani kwa ahadi ya Mwenyezi Mungu. Adui aliyeumia ameleta na ataleta uwezo wake wote katika medani. Tunapaswa kuchukua tahadhari, kuwa na hekima, ushujaa na kutambua fursa zilizopo. Ni kwa njia hiyo ndipo njama zote za adui zitafeli na kuambulia patupu. Katika miaka 30 iliyopita, maadui hasa Marekani na Uzayuni wametumia uwezo wote walio nao lakini wamefeli. Siku za usoni pia hali itakuwa hiyo hiyo. InshaAllah.
Ukali wa vitendo vya adui aghalabu unaonyesha udhaifu wake na namna asivyokuwa na tadbiri. Hebu tupia jicho hali ya mambo Palestina na hasa Ghaza. Harakati zisizo na huruma na za kikatili za adui huko Ghaza ambazo hazijawahi kushuhudiwa ila kwa uchache katika historia ya ukatili wa mwanaadamu ni jambo linaloashiria udhaifu wake katika kukabiliana na irada imara ya wanaume, wanawake na watoto ambao kwa mikono mitupu wamesimama kidete dhidi ya utawala Ghasibu na muitifaki wake yaani dola kubwa la Marekani. Wametupilia mbali takwa la maadui ambalo ni kukataa serikali ya Hamas. Baraka za Mwenyezi Mungu zilimiminikie taifa adhimu linaloonyesha istikama huko Ghaza. Wananchi wa Ghaza na serikali ya Hamas wamezipa maana halisi aya zifuatazo za Qur'an tukufu zinazosema:
وَلَنَبْلُوَنَّكُمْ بِشَیْءٍ مِّنَ الْخَوْفْ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِّنَ الأَمْوَالِ وَالأنفُسِ وَالثَّمَرَاتِ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ
الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ قَالُواْ إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَیْهِ رَاجِعُونَ
أُوْلَئِكَ عَلَیْهِمْ صَلَوَاتٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَرَحْمَةٌ وَأُولَئِكَ هُمُ الْمُهْتَدُونَ
"Hapana shaka tutakujaribuni kwa chembe ya khofu, na njaa, na upungufu wa mali na watu na matunda. Na wabashirie wanao subiri. Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea. Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola wao Mlezi na rehema. Nao ndio wenye kuongoka. (2: 155-157) na
لَتُبْلَوُنَّ فِی أَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ وَلَتَسْمَعُنَّ مِنَ الَّذِينَ أُوتُواْ الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ وَمِنَ الَّذِينَ أَشْرَكُواْ أَذًى كَثِيرًا وَإِن تَصْبِرُواْ وَتَتَّقُواْ فَإِنَّ ذَلِكَ مِنْ عَزْمِ الأُمُورِ
Hapana shaka yoyote mtapata misukosuko katika mali zenu na nafsi zenu, na bila ya shaka yoyote mtasikia udhia mwingi kutokana na walio pewa Kitabu kabla yenu na wale walio shiriki. Na ikiwa mtasubiri na mkamchamngu basi hakika hayo ni katika mambo ya kuazimia. (3:186)
Ukweli utapata ushindi wa mwisho katika mapambano hayo ya haki na batili na ni taifa hilo lililodhulumiwa na lenye subira la Palestina ndilo ambalo hatimaye litapata ushindi dhidi ya adui.
وَكَانَ اللَّهُ قَوِیًّا عَزِيزًا
Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na uweza. (33:25)
Hata leo mbali na adui kushindwa kuvunja mapambano ya Wapalestina katika medani ya kisiasa amepata pia pigo kubwa pamoja na kuwa amekuja kwa nara za uongo za uhuru na demokrasia na kutetea haki za binaadamu. Jambo hilo limeufedhehesha sana utawala za Marekani na aghlabu ya tawala za Ulaya na wala haziwezi kulipiza fedheha hiyo katika siku za hivi karibuni. Utawala usio na aibu wa Kizayuni umepata doa jeusi zaidi na baadhi ya tawala za Kiarabu zimepoteza heshima na itibari katika mtihani huu wa ajabu.
وَسَیَعْلَمُ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَیَّ مُنقَلَبٍ یَنقَلِبُونَ
Na wanaodhulumu watakuja jua mgeuko gani watakaogeuka. (26:227).
Sayyid Ali Husainy Khamenei
4 Dhil-Hijjah 1429/
3 Disemba 2008. 331066