IQNA

Sheikh wa al Azhar aliomba kukutana na Peres

12:12 - December 09, 2008
Habari ID: 1717463
Gazeti la Ma'ariv linalochapishwa katika utawala ghasibu wa Israel limeandika kuwa Sheikh wa al Azhar Muhammad Sayyid Tantawi ndiye aliyeomba kukutana na kupeana mkono na Rais wa Israel Shimon Peres wakati wa mkutano wa Mazungumzo ya Dini Mbalimbali mjini New York, Marekani wiki kadhaa zilizopita.
Gazeti la Ma'ariv limeandika katika makala yake iliyochambua tukio la kupeana mikono kati ya Sheikh wa al Azhar na Shimon Peres kwamba tukio hilo lilifanyika kutokana na ombi la Muhammad Tantawi.
Makala hiyo imesema: Tantawi ambaye anamjua vyema Rais wa Israel Shimon Peres alimsogelea huku akitabasamu na kuumpa mkono.
Katika upande mwingine Tantawi amekadhibisha vikali madai ya gazeti hilo la kusema, makala hiyo imeandikwa na maghasibu wanaoikalia kwa mabavu Palestina kwa kipindi cha miaka sitini.
Kiongozi huyo wa moja ya taasisi kubwa zaidi za Kiislamu duniani amekuwa chini ya mashinikizo makali ya Waislamu kote duniani baada ya kupeana mkono na kiongozi wa utawala unaoendelea kuwaangamiza wananchi wasiokuwa na hatia wa Palestina. Wabunge wa Misri wamemtaka Tantawi ajiuzulu. 331633
captcha