IQNA

Kongamano la Mazungumzo ya Uislamu na Ukristo mjini Istanbul

15:32 - December 15, 2008
Habari ID: 1719489
Kongamano la kimataifa la Mazungumzo ya Uislamu na Ukristo limeanza leo mjini Istanbul, Uturuki likihudhuriwa na viongozi wa masuala ya kidini na kisiasa wa Kiislamu na Kikristo kutoka nchi mbalimbali.
Mwandishi wa IQNA nchini Uturuki ameripoti kuwa, kongamano hilo la siku mbili linasimamiwa na kituo cha kimataifa cha Balemy cha Sweden na kundi la Diyar Palestine.
Viongozi wa kidini na wabunge wa Uturuki na nchi kadhaa za Ulaya na Mashariki ya Kati wanajadili na kubadilishana mawazo kuhusu njia za kuimarisha mazungumzo kati ya wafuasi wa dini za Uislamu na Ukristo. 333672
captcha