IQNA

Mbunge wa Austria aliyeutusi Uislamu kuadhibiwa

18:39 - December 15, 2008
Habari ID: 1719540
Mbunge mmoja wa Austria ambaye hivi karibuni alitoa matamshi ya kuzivunjia heshima itikadi za Kiislamu amekosolewa na bunge la nchi hiyo.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, bunge la Austria limemuondolea kinga ya kisheria mbunge huyo mbayo alimvunjia heshima Mtume wa Uislamu.
Susan Winter wa chama cha mrengo wa kulia chenye misimamo mikali cha Austrian Freedom Party (FPÖ) anatazamiwa kufunguliwa mashataka katika siku zijazo.
Jumuiya ya Ulaya ya Kupinga Ubaguzi (ENAR) imelaani matamshi yaliyotolewa na Winter na kutoa wito kwa wanasiasa wote Ulaya kujizuia kutoa matamshi yanayochochea hisia za kidini . 333569



captcha