IQNA

Kikao cha 11 cha dini chaanza mjini Roma

12:39 - December 18, 2008
Habari ID: 1720155
Kikao cha kila mwaka cha dini mbalimbali kimeanza kazi zake katika mji mkuu wa Italia, Roma kikihudhuriwa na wanafikra wa Kiislamu na Kikristo.
Kikao hicho kinasimamiwa na viongozi wa Vatican na Jumuiya ya Kimataifa ya Ulinganiaji wa Kiislamu.
Miongoni mwa maudhui muhimu za kikao hicho ni mjadala juu ya 'nyadhifa za kidini', 'nyadhifa za kijamii na kitamaduni' na 'mpango wa kuitisha vikao vya dini mbalimbali wakati wa migogoro'.
Kikao hicho kinafuatia kile cha mwezi uliopita mjini Vatican ambacho kilifanyika kwa shabaha ya kuimarisha maelewano na amani baina ya dini mbili kuu za Kiislamu na Kikristo.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa Waislamu wanaunda karibu jamii ya watu bilioni moja na nusu huku Wakristo wakiwa karibu bilioni mbili kote duniani. 334657

captcha