Waandamanaji hao walikuwa wamebeba mabango ya kulaani jinai za utawala wa Kizayuni ambao umekuwa ukitekeleza sera za kikatili na zilizo kinyume cha misingi ya ubinadamu. AIdha wamelaani Marekani kwa kuendelea kuupa himaya utawala haramu wa Israel katika jinai zake hizo dhidi ya Wapalestina.
Katika maandamano hayo, Mashia wa Qatif pia walikuwa wamebeba picha za Sayyid Hassan Nasrullah kiongozi wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon. Aidha waandamanaji hao wameunga mkono kitendo cha Muntadhir Zaydi mwandishi habari Muiraqi aliyemvurumishia viatu rais Bush wa Markekani. Waislamu hao wanaofuata madhehebu ya Shia mjini Qatif wamemshukuru Sayyid Nasrullah kwa uungaji mkono wake kwa Wapalestina wa Ghaza na wametoa wito kwa Misri kufungua kituo cha mapakani cha Rafah ili kuwaruhusu Wapalestina wa ghaza kuingia Misri kuchukua bidhaa wanazohitajia kila siku. 336054