IQNA

Kongamano la kuvunja mzingiro wa Gaza mjini Tehran

12:11 - December 21, 2008
Habari ID: 1720992
Naibu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu wa Kishia wa Lebanon ameyataka mataifa yote ya Kiarabu na Kiislamu kufanya juhudi za kuitisha kongamano la wananchi katika mojawapo ya miji ya Tehran, Makka au Cairo kwa shabaha ya kuchunguza hali ya Palestina na jinsi ya kuvunja mzingiro wa Gaza.
Ayatullah Sheikh Abdul Amir Qublan amesema: Waislamu wote wanapaswa kufanya juhudi za kuwaokoa wananchi wanaodhulimiwa wa Palestina na kwamba haijuzu kunyamaza kimya mbele ya jinai za Israel dhidi ya wakazi wa eneo hilo.
Naibu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu wa Kishia la Lebanon amesema kuwa, utawala haramu wa Israel umeelekeza silaha zake zote kwa watu wasiokuwa na hatia na kutishia usalama wao.
Amezungumzia pia hali ya ndani ya Lebanon na akasema: Nchi hiyo ni moja ya nchi zilizosimama kidete dhidi ya maghasibu wa Kizayuni. Amewataka wanasiasa na maulama kumuogopa Mwenyezi Mungu na kuwahudumia wananchi. 335735
captcha