Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA mjini Beirut, Allamah Sheikh Muhammad Hussein Fadhlullah Marjaa wa Waislamu wa Kishia nchini Lebanon alisisitiza hayo Jumatatu tarehe 22 Disemba katika mkutano na wanachama wa Bunge la Kuwait na kuongeza kuwa: “Minasaba ya Kiislamu na juu ya yote mwanzo wa mwezi wa Hijria wa Muharram na kumbukumbu ya Ashura mbali na hotuba na mahafali mengine kwa hakika ni fursa ya kuimarisha Umoja wa Kiislamu”.
Marjaa huyo wa Kiislamu wa Lebanon ameongeza kuwa kuna udharura kwa Wakuwaiti kushirikiana ka ajili ya maslahi ya nchi yao.
Allamah Fadhlullah amesisitiza juu ya umuhimu wa kufikiwa umoja wa Kiislamu ndani ya Kuwait na kuepuka tabia na mienendo ya chuki za kimadhehebu.
Mwishoni mwa kikao hicho hicho, mwanachuoni huyo wa Lebanon ametaka kuwepo ushirikiano baina ya makundi mbalimbali ya Kiislamu ya Kishia na Kisuni nchini Kuwait kwa lengo la kuvunja njama za maadui za kuleta mgawanyiko miongoni mwa Waislamu. 337310