Kwa mujibu wa Askofu Mkuu wa Wakatoliki mjini Quds Fouad Tawal, Papa Benedict wa 16 atakutana na wakaazi wa mji huo katika safari yake hiyo pamoja na kushiriki katika misa ya pamoja. Aidha atafahamishwa kuhusu hali mbaya ya maisha katika mji huo unaokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Askofu Mkuu Fouad Tawal amesema mbali na kuzuru Quds, Papa pia atatembelea eneo la Palestina la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, na miji mingine ya Palestina ya an-Nāṣirah , Bait Lahm.
Hii itakuwa safari ya kwanza Mashariki ya Kati kwa PapaBenedict mwenye asili ya Ujerumani ambaye alichaguliwa mwaka 2005.
Papa Paule VI alikuwa, kiongozi wa kwanza wa wakatoliji duniani kutembelea ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina. Wa mwisho alikuwa Papa John Paul wa pili aliyetembelea ardhi hizo takatifu mwaka 2000. 338477