IQNA

Programu ya "Kuujua Uislamu" katika maonyesho ya Doha

11:35 - December 28, 2008
Habari ID: 1723579
Viongozi wa ukurasa wa mtandao wa intaneti wa Islam Online wanaoshiriki katika Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Doha mji mkuu wa Qatar wameandaa programu ya moja kwa moja ya maswali na majibu yenye anwani "Ujue Uislamu".
Kwa mujibu wa gazeti la Peninsula, afisa mwandamizi wa mtandao wa intaneti wa Islam Online Ustadh Salahuddin ambaye pia alikuwa mwendeshaji wa programu hiyo tangu mwanzo wa maonyesho, kila siku amekuwa akijibu maswali mbalimbali kuhusu Uislamu.
Lengo la mpango huo limetajwa kuwa ni kutoa maelezo sahihi na kamili kuhusu Uislamu.
Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Doha yalifunguliwa Disemba 27, 2008 na yataendelea hadi Januari 3, 2009.
Kuna vibanda 74 katika maonyesho hayo ambayo yametajwa kuwa makubwa zaidi kuwahi kufanyika nchini Qatar. Washiriki ni kutoka nchi 21 na wanaonyesha anwani 28,164 za vitabu vya Kiarabu na lugha nyinginezo. 338781
captcha